Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali ofisini
kwake juu ya kusambaa kwa habari inayohusu uwepo wa kiwanda cha kutengeneza uume bandia.
..................................
Siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na
kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.
Akizungumza na Wandishi wa habari ofisini kwake Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa
mtandaoni juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto
huku akiwataka wananchi kuondokana na dhana potofu za kuchukua habari za
mitandaoni na kuupotosha umma.
“Naomba niende kuwaomba radhi watanzania kwa ajili ya jambo
ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya kijamii hasa nchi ya jirani zetu
hapo Kenya" alisema Kasesela.
Kasesela aliwataka watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu
na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi
na yenye tija kwa maslahi ya Taifa.
“Jamani ile habari ilitungwa na ni habari ya hovyo sana kwa
kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema kwenye chombo chochote kile kwenye
vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya
kupuuza tu” alisema Kasesela.
Kasesela amewashauri watanzania kuhakikisha wanafatilia
taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye
kujenga katika jamii inayomzunguka.
“Kwa sasa habari nyingi ambazo zinazungumzwa ni habari
ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio
maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio kweli”
alisema Kasesela.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard
Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine kusambaza taarifa
zisizo za kweli na kuongeza kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa
vya elimu ya mapambano
dhidi ya Ukimwi.
No comments:
Post a Comment