NA
HADIJA HASSAN, LINDI
JESHI
la polisi mkoa wa lindi limefanikiwa kupunguza makosa ya usalama wa barabarani
kwa asilimia 26 kwa kipindi cha miezi mitatu januari hadi machi 2019
ukilinganisha na makosa yaliyotendeka kwa kipindi kama hicho mwaka uliopita wa
2019
Hayo
yameelezwa na kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Pudensiana Protas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hivi
karibuni ofisini kwake
Kamanda
Protas alisema kuwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2019 makosa ya Barabarani
yaliyoripotiwa yalikuwa 7,096 ikilinganishwa na makosa yaliyoripotiwa kwa
kipindi kama hicho mwaka 2018 ambapo yalikuwa 9,550 hivyo kuwa na upungufu wa
matukio 2,454 sawa na asilimia 26
Akieleza
sababu za kupungua kwa makosa hayo Kamanda Protas alisema kuwa makosa hayo
yamepungua kutokana na kufanyika kwa oparesheni za mara kwa mara za kushitukiza
kwa kukamata Magari mabovu yanayoendelea kuendeshwa pamoja na yale yanayokiuka
sheria za barabarani
Hata
hivyo kamanda Protas alisema kuwa katika kipindi hicho cha Mwezi Januari
hadi Machi 2019 pia makosa ya jinai yaliyoripotiwa yamepungua kwa asilimia 8%
kutoka1,687 kwa mwaka 2018 hadi kufikia 1,556 kwa 2019 ukilinganisha na
makosa yaliyofanyika kwa kipindi kama hicho na kufanya upungufu wa makosa
131
No comments:
Post a Comment