Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto)akiongea jambo wakati alipofanya ziara ya
kukagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
(General). Kulia ni katibu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula.
..............................................
Na
WAMJW-Dodoma
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi
kutoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje
(OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Waziri
Ummy ametoa ahadi hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la
mama na mtoto (Maternity Block) katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya
utoaji huduma kwa akina mama wajawazito na watoto.
“Ninaahidi
kutoa Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la OPD ya kisasa yenye
uwezo wa kupokea wagonjwa wengi zaidi tofauti na OPD iliyopo sasa”. Amesema
Waziri Ummy.
Waziri
Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kurekebisha na kufanya maboresho katika
baadhi ya maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuyapa majina majengo yote ya Hospitali hiyo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa
pindi wanapotaka kupata huduma katika majengo tofauti.
Aidha,
Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kujenga ghorofa ambayo itakua
maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee yenye uwezo wa kulaza watoto wengi
sambamba na chumba cha uangalizi maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda
(Intensive Neonatal Care Unit) na wale wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema Wizara
itaendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali hiyo katika kutatua changamoto
mbalimbali zilizoonekana katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja kuongeza
watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji.
“Naomba niwaahidi tutaongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kuziba
mapungufu yanayoonekana, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika Hospitali hii
inayotegemewa na watu wengi wa Dodoma na kutoka maeneo ya jirani”. Amesema Dkt.
Chaula.
Hata
hivyo Dkt. Chaula amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kushirikiana ili waweze
kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo.
Katika
ziara hiyo iliyoenda sambamba na siku ya Afya Duniani imejumuisha viongozi
mbalimbali wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbaga
wameondoka na azimio la kufanya maboresho katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja
na kujengwa kwa jengo maalum la kupokea wageni mbalimbali wanaokuja Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea hotuba kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Benzi wakati walipofanya ziara
ya kukagua jengo la mama na mtoto (Maternity Block). Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara
hiyo Dkt. Zainab Chaula na nyuma viongozi wengine wa Wizara na Hospitali.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na mama aliyejifungua katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la
Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.
Jengo jipya la Mama na Mtoto (Maternity Block)
lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
No comments:
Post a Comment