Baadhi
ya vijana kutoka katika halmashauri ya mji Kibaha ambao wameshiriki katika
mafunzo ya ujasiriamali wakiwa wanasikiliza mada ambazo zilizokuwa zikitolewa
na wawezeshaji kutoka TECC pamoja na SIDO.
...........................................
VICTOR
MASANGU, KIBAHA
VIJANA wapatao 35 katika
halmashauri ya mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani ambao walikuwa
wanakabiliwa na wimbi la ukosefu wa upatikanaji wa ajira wamepatiwa
mafunzo maalumu ya ujasiriamali kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na
kuondokana na tatizo la umasikini.
Hayo wamebainishwa na Meneja wa
Taasisi ya ujasiramali na ushindani Tanzania (TECC) Anna
Manuti wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku 11 ya ujasiliamali kwa
baadhi ya vijana waliopo katika halmashauri ya mji Kibaha ambayo yameandaliwa
kwa lengo la kuwapa mbinu mbali mbali zitakazoweza kuwasaidia kujiajiri na
kuacha kuwa tegemezi.
Aidha Meneja huyo amebainisha kuwa
katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili baadhi ya vijana wameamua
kuwakutanisha vijana hao kwa lengo la kuwawezesha kwa kuwapatia elimu
ambayo itawapa fursa ya kuanzisha biashara zao wenyewe lengo likiwa ni
kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
“Hii programu ya kuwawezesha vijana
mafunzo ya ujasiriamali tunaifanya kwa kipindi cha miaka miaka mine na
inatarajia kumalizika mwaka 2020 na kwa sasa huu ni mzunguko wa
sita ambapo katika halmashauri ya mji wa kibaha vijana wapatao 35 wamepata
fursa ya kupatiwa mafunzo haya ambayo yatawea kuwasaidia kuweza kujiajiri wao
wenyewe,”alisema Anna.
Kwa upande wake Meneja wa shirika
la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Behata Minga
amesema programu ya kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali
ya ujasiriamali itawasaidia vijana kujiajiri wao wenyewe
kutokana kuanzisha viwanda vidogovidogo lengo ikiwa ni kujikwamua
kiuchumi na kupambana na wimbi la umasikini.
“Kwa kweli mradi huu wa kuwapatia
mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana hasa
katika Mkoa wetu wa Pwani na sisis kama Sido tutahakikisha tunashirikiana
bega kwa beda na taasisi hii ya TECC ambayo imefanikisha kuwakusanya vijana
hawa na kuwapa mahalifa ambayo yatawasaidia kupata ajira pamoja na kuanzisha
viwanda vidogividogo,”alisema Mlinga.
Nao baadhi ya vijana ambao wameshiriki
katika mafunzo hayo akiwemo Selemani Shabani pamoja na Azaria Namga wamesema
kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na
ajira, ukosefu wa mitaji ya biashara hivyo wameiomba serikali ya
awamu yatano kuwasaidia kwa halina mali ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.
MRADI huo wa kuwawezesha vijana
kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali unatekelezwa katika mikoa mine ya
Jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara pamoja na Pwani ambapo hadi sasa
katika mikoa yote hiyo vijana wapatao 894 wamenufaika na programu
hiyo ambayo inatarajia kumalizika mwaka 2020.
Mwezeshaji
wa semina hiyo ambaye pia ni Afisa kutoka Shirika la kuhudumia viwanda
vidogovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Merina Mkuchu akitoa maelekezo kwa
vijana hao ambao wameshirki katika mafunzo ya ujasiriamali.
Meneja
wa Taasisi ya ujasiramali na ushindani Tanzania (TECC) Anna
Manuti akizungumza jambo na vijana ambao wameshiriki wakati
wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo ya ujasiliamali ambayo yamefanyika katika
katika kata ya maili moja Wilayani Kibaha.
Mmoja
wa wawakilishi wa vijana kutoka katika halmashauri ya mji Kibaha Shauri Yomba
Yomba akizungumza na washiriki ambao hawapo pichani kuhusiana na umuhimu wa
mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yameandaliwa na taasisis ya
Meneja
wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Behata Minga
akizungumza jambo katika ufunguzi wa mafunzo ya
ujasiliamali kwa vijana wa halmashauri ya mji Kibaha
(PICHA
ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment