Thursday, April 4, 2019

Mbio za sokoine memorial kuitikisa Arusha, Wakazi washauriwa kufunga maduka yao kuitafuta afya yao





Siku ya jumamosi itakuwa ni siku ya kipeke katika Jiji la Arusha ambapo wanamichezo wa riadha pamoja na wasanii mbalimbali watakapochuana katika mbio za kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa Zamani Edward Molinge Sokoine.

Katika mbio hizo ambazo zimeelezwa kushirikisha watu mbalimbali kutoka ndani ya Nchi na Nje , zinatarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu wa sasa, Mh. Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, msanii steve Nyerere amesema mbio hizo zitakuwa za aina yake kufuatia wasanii mbalimbali kujipanga kuhakikisha wanashindana ipasavyo katika mbio hizo.

Amesema imezoleka kuona wasanii wakishambulia jukwaa lakini Jumaso mambo yatakuwa tofauti kwa sababu watakimbia mbio hizo kwa shaukuwakikumbuka kumbukizi ya shujaa wetu Hayyat Edward Sokoine.

“Sisi kama wasanii wanauzalendo kwanza tuikiungana na familia ya sokoine, pamoja na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa rais wetu mpendwa Mh. John Magufuli sambamba na makamu wa RAIS mama Samia sululu tunaungana na wenzetu wa Arusha kumuenzi Waziri Mkuu wa Zamani Sokoine” alisema 

Aidha Steve Nyerere amewataka wakazi wa Arusha na viunga vyake kujitokeza katika mbio kushuhudia kumbukukizi hiyo muhimu, na kwamba Ireen Uwoya atamkimbiza Waziri mkuu. Ni mwendo wa buradi siku hiyo. Mimi mwenyewe nachomoka vibaya mno yaani kipenga kikifanya puu tayari nishamaliza mbio yaani utaniona Iringa.

Siku hiyo fungeni maduka yenu mje mtafute afya zenu, iku hiyo ni siku muhimu kiwa ajili ya kumuenzi kiongozi wetu.

Mjumbe wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo alisema mbio hizo zitashirikisha wanariadha nyota nchini na wengine kutoka nje ya nchi ambao watakuwa na vibali kutoka kwenye M mashirikisho ya riadha ya nchi wanazotoka.
“Mashindano yataanzia kwenye mnara wa Clock Tower Arusha na yatamalizikia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo zitapokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema.
Naye Katibu wa Kamati ya Ufundi ya RT, Rehema Killo, alisema kutakuwa na mbio za kilomita 21 (Wazalendo nusu marathoni) ambazo washindi kwa wanaume na wanawake kila mmoja ataondoka na Shilingi 1,000,000.
Alisema mshindi wa pili atazawadiwa Sh 800,000 na wa tatu Sh 600,000 huku zawadi zikitolewa kwa washindi 15 wa kwanza huku washindi 500 wa kwanza watapewa medali ya ushiriki.
Awali mbio hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza miaka minne iliyopita na msimu huu zitafanyika kwa mara ya pili ambapo zinalenga kumuenzi hayati Sokoine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika mbio hizo za kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine itakayoadhimishwa Aprili 12, mwaka huu.


No comments:

Post a Comment