Picha hii kutoka maktaba yetu.
NA HADIJA HASSAN- LINDI.
NA HADIJA HASSAN- LINDI.
ZAIDI
ya Wakulima 700 wa Zao la Korosho kutoka Chama cha Msingi Cha Ushirika Mtua na Kiwalala
AMCOS vya chama Kikuu cha ushirika Lindi Mwambao, Halmashauri ya Wilaya ya
Lindi Mkoani humo hawajalipwa fedha zao Licha ya Serikali kuahidi mpaka
ifikapo Tarehe 31 mwezi machi 2019 itakuwa imelipa fedha zote kwa wakulima hao
Hayo
yameelezwa kwa nyakati tofauti na waandishi wakuu wa vyama hivyo
katika ofisi zao walipokuwa wanazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG jana Aprili 2
ilipotembelea kijijini hapo
Akizungumza
na Bagamoyo kwanza Blog mwandishi wa chama cha msingi cha ushirika
Kiwalala AMCOS Mshamu Chindamba alisema kuwa katika msimu wa mauzo wa
mwaka 2018/19 chama chake kilikusanya jumla ya kg 517,953 ambapo kati ya hizo
kg 294,546.19 sawa na tsh. 972,002,427 zililipwa kupitia mfumo wa serikali na
kg 10,000 zilinunuliwa na wahindi katika mnada wa kwanza
Hata
hivyo alisema kati ya hizo kg 111,160 za wakulima wa kilo chini ya kg 1500 sawa
na tsh. 336,830,678 na kg 102,246 sawa na sh. 337,411,800 za wakulima wenye
kilo zaidi ya kg 1500 hawajalipwa
Nae
mwandishi Mkuu wa chama cha Msingi Mtua Amcos Abdallah Chikapoka alisema
kuwa katika msimu wa mauzo 2018/19 Chama chao kilikusanya jumla ya
korosho kg. 558,939 ambapo kati ya hizo kg 50,000 ziliuzwa
katika minada ya wahindi na kg.508,939 ziliingizwa kwenye mfumo wa malipo ya
Rais sawa na thamani ya sh.1,679,498.700
Chikapoka
alisema kati ya hizo kg 431,288 zenye thamani y ash.1,423,250.400
zililipwa huku kg77,651 sawa na tsh. 256,248,300 zikiwa bado hazijalipwa
ambapo kati ya hizo tani 1162 za wakulima wenye kilo chini ya 1500 na kg. 76489
ni za wakulima walio na kilo zaidi ya 1500
Awali
wakizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG baadhi ya wakulima wa zao hilo wakazi wa
Kata ya Kiwalala na kijiji cha Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani humo
Daudi Namteka, Rukia Maarifa, Abdalla Ndambilejao na Esha Abdallah
wameonyesha kusikitishwa juu ya ahadi zinazotolewa na viongozi wa
Serikali juu ya malipo ya korosho zao
“
mwaka huu hali ya hewa haikuwa mzuri sana kama miaka ya nyuma hivyo sikupata
korosho nyingi nilipata kama Tani 9.5 hivi kati ya hizo tani 1.5 niliuza katika
chama cha msingi Mandwanga AMCOS na kg 8880 niliuza katika chama cha msingi
Kiwalala Amcos ambazo mpaka sasa sijapata fedha zangu zote kinachonisikitisha
mpaka sasa hivi kutokana na tamko la Serikali lililotolewa na waziri wa kilimo
wiki mbili zilizopita tulipewa matumaini kwamba fedha ipo na mpaka tarehe 31
mwezi machi wakulima wote tutakuwa tumeshalipwa fedha zetu lakini mimi mpaka
jana nilienda Bank kuangalia salio lakini sijakuta kitu chochote wala
sijajua tatizo lipo wapi ?sasa sisi wakuliam tumebaki na maswali yasiyokuwa na
majibu yake” Alisema Abdallah Mshamu
“Nimeuza
korosho zangu toka tarehe 26 mwezi wa 11 adi leo hii sijalipwa ela yangu ,
shamba langu chafu mimi mwenyewe hali yangu ya maisha ni ngumu maana nilikuwa nategemea
hiyo ela nifanyie mpango mingine ya kupatia fedha ili niendeshe maisha yangu
alafu nashangaa watu wenye kilo kidogo walisema tutalipwa mapema lakini mimi
sijalipwa mpake leo na kilo zangu hazijazidi hata kilo 1500 tatizo hili liko
wapi ? nimechoka kumaliza maliza nauli kufuatilia ela yenyewe hiyo” Alieleza
Rukia Maarifa
“Mara
ya kwanza waziri Mkuu kasimu majaliwa alisema mpaka tarehe 15 mwezi wa pili
wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao tulivumilia tukawa watulivu tarehe
hile ikapita juzijuzi waziri wa kilimo nay eye akatoa kauli yake kwamba mpaka
tarehe 31 mwezi wa tatu wote tutakuwa tumelipwa rohozetu zikawa kwatuuuu
kusuburi siku hiyo lakini mpaka inapofikia leo hatujalipwa sasa tunaanza kukosa
imani na serikali yetu tunajua nia ya Rais wetu ilikuwa mzuri lakini huwenda
watendaji wake hawafanyi vizuri” Alifafanua Abdallah Ndamilejao
Ukistaajabu
ya musa utayaona ya filauni wakati BAGAMOYO KWANZA ipo katika pita pita zake ikamkuta
kikongwe aliekaa zaidi ya masaa saba katika chama cha mtua AMCOS akiwashinikiza
viongozi wa Chama hiko kumlipa fedha zake za korosho
“Hapa
nimekuja kwa wakuu wa hapa wanilipe ela zangu tu maana nimechoka kuzungushwa
mpaka sasa nimeshaenda Lindi mara kumi na mbili Bank kufuatilia malipo
yangu lakini naambiwa nije kwa viongozi wangu wa chama , kila nikienda kule
natumia nauli tena nakopa kwa majirani mpaka sasa imeshafika laki moja ambayo
nadaiwa sasa si ela yenyewe yote mwisho nikalipa madeni tuu mimi” aleelezea
Esha Abdallah
Hata
hivyo kufuatia kuchelewa kwa malipo ya wakulima wa korosho Rais Magufuli
alipokuwa akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Mtwara jana aprili O2, 2019
alitoa siku tano kwa wizara ya kilimo kuhakikisha inawalipa wakulima wote wa
korosho
Mwandishi Muu wa chama cha msingi cha ushirika Kiwalala AMCOS, Mshamu Chindamba alipokuwa anazungumza na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake.
Mkazi
wa kijiji cha Mtua Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani Lindi, Esha Abdallaah , akionyesha stakabadhi ya
kuwasilisha korosho zake katika chama cha msingi Mtua AMCOS
PICHA NA HADIJA HASSAN WA BAGAMOYO KWANZA BLOG-LINDI
PICHA NA HADIJA HASSAN WA BAGAMOYO KWANZA BLOG-LINDI
No comments:
Post a Comment