Wahudumu
wakitoa huduma ya vipimo vya malaria kwa wananchi waliofika uwanja wa majengo
mjini Bagamoyo leo Aprili 25, 2019 katika maadhimisho ya siku ya Malaria
duniani.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Bagamoyo, Athumani Stili akimuakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
.................................
Wananchi
wilayani Bagamoyo wametakiwa kuwa na tabia ya kufika hospitali kupata pindi
wanapohisi dalili za homa ili kujua kama ni Malaria au la.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Bi Zainabu Kawawa katika
maadhimisho ya siku ya Malaria duniani kupitia hutuba iliyosomwa kwa niaba yake
na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Bagamoyo, Athumani Stili.
Amesema
baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kutumia dawa bila ya kupima hali
inayopelekea kupata madhara pale ugonjwa unaposhika kasi.
Alisema
sio kila homa ni Malaria hivyo ni vyema unapojisikia maumivu ya mwili kufika
kwa wataalamu wa afya ili ujue kitu gani kinakusumbua.
Awali
akisoma Taarifa mbele ya Mgeni rasmi Mratibu wa Malaria wilaya ya Bagamoyo Dkt.
Zena Mtajuka amesema miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo wilayani humo
ni pamoja na Malaria.
Alisema
katika kipindi cha mwaka 2018 asilimia tano ya wagonjwa waliohudhuria kitengo
cha nje (OPD) wamekutwa na Malaria huku wagonjwa waliolazwa ni asilimia 7.9
ndio waliokutwa na Malaria.
Alisema
ugonjwa wa Malaria huleta athari kwenye jamii na taifa kwa ujumla kwakua kipato
kinashuka kutokana na watu kuugua malaria.
Aidha,
alisema ili kufikia lengo la taifa katika kudhibiti Malaria, Halmashauri ya
Bagamoyo imejipanga katika kutekeleza kazi mbalimbali za kupambana na ugonjwa
huo.
Alisema
miongoni mwa kazi hizo ni upatikanaji wa matibabu sahihi ya ugonjwa wa malaria
katika vituo vyote 27 vilivyopo katika Halmashauri hiyo, kupatikana kwa
Vyandarua vyenye viuatilifu kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja
wakati wa chanjo ya kwanza ya surua.
Taasisi
ya Utafiti wa afya ifakara (ihi) tawi la Bagamoyo ndio waliodhamini maadhimisho
hayo na kutoa elimu mbalimbali kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Malaria.
Katika
maadhimisho hayo ambayo kwa Bagamoyo yamefanyika uwanja wa Majengo ambapo
wananchi walipata huduma ya kupima malaria pamoja Virusi vya Ukumwi bila ya
malipo.
Siku
ya Malaria duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Aprili 25 ambapo ujumbe wa
mwaka huu "Ziro Malaria huanza na mimi"
Mwenyekiti
wa Bodi ya Afya Halmashauri ya Bagamoyo, Roswita F. Kasikila akizungumz katika
maadhimisho hayo yaliyofanyika uwanja wa majengo mjini Bagamoyo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally issa akizungumza katika
maadhimisho hayo yaliyofanyika uwanja wa majengo mjini Bagamoyo.
Kiongozi
wa wanasayansi kutoka Taasisi
ya Utafiti wa afya ifakara (ihi) Dkt. Ally Olotu akizungumza katika
maadhimisho hayo yaliyofanyika uwanja wa majengo mjini Bagamoyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Bagamoyo, Athumani Stili akimuakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, ( wa pili kushoto, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally issa, wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Halmashauri ya Bagamoyo, Roswita F. Kasikila na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa afya ifakara (ihi) tawi la Bagamoyo Dkt. Aseline Charles.
Kaimu
Mganga Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Salvio Wikes kizungumza katika
maadhimisho hayo yaliyofanyika uwanja wa majengo mjini Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment