Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu, amefanya kikao kazi maalumu na
Watumishi wa Halmashauri kuwaelekeza na kuwakumbusha maagizo mbalimbali ya
Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Watumishi hao wapatao 250 wa makao
makuu na watendaji wa Kata waliohudhuria mkutano huo walikumbushwa juu ya
uadilifu katika utumishi wa Umma, weledi, kufuata
utaratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao, kuzingatia lishe na usafi wa kila
mtumishi binafsi, mada zilizowasilishwa kwa Watumishi hao na Mkurugenzi
mtendaji akisaidiana na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
Akizungumza na Watumishi hao
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu amewasisitiza
Watumishi hao kuzingatia utunzaji wa Afya zao kwa kula vizuri, kwani mtumishi
anayekula vizuri na mwenye Afya njema na uwezo mkubwa zaidi wa kusikiliza,
kuyaelewa na kuyafanyia kazi maagizo mbalimbali ya Serikali.
"Serikali inafanya kazi kwa
vipaumbele, na katika masuala ya Watumishi, inasisitiza Watumishi wa Umma
kuhakikisha wanazingatia masuala ya lishe, kwa kula mlo kamili kila siku ili
kuimarisha Afya zao na kujiongezea uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na weledi
kwani Chakula kina uwezo wa kumpa mtu nguvu, Afya na wakati mwingine Chakula ni
dawa"
"Nawasihi sana hakikisheni mnatenga muda wa kula chakula mnapokuwa katika
kutimiza majukumu yenu ya kila siku, mishahara mnayopokea, muitumie pia kwa
ajili ya kupata chakula bora ninyi na familia zenu, sio mnatumia mshahara wote
kukopa katika taasisi mbalimbali za fedha na kusahau kabisa kama kuna umuhimu
wa kujihakikishia kupata mlo wa kila siku kupitia mshahara huo huo"
Alisema Bi. Fatuma Latu
Watumishi walioshiriki kikao hicho
pia walipata nafasi ya kuuliza maswali na kuwasilisha kero wanazokumbana nazo
wakati wakitimiza majukumu yao ya kila siku ambapo baadhi yao walizungumzia
kero ya kutopandishwa madaraja kwa muda mrefu, malipo ya stahili mbalimbali na
changamoto ya upungufu wa watumishi, na mambo hayo yote yalitolewa ufafanuzi wa
kina na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Wakuu wa Idara.
Mkurugenzi Mtendaji ameanzisha
utaratibu wa kukutana na Watumishi wa Halmashauri mara moja kwa Mwezi, kwa ajili
ya kuwapa maelekezo mbalimbali ya Serikali na kusikiliza kero za watumishi hao,
lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika utendaji kazi za Halmashauri.
Sehemu ya Watumishi wa Halmashauri ya Bagamoyo wakiwa kwenye kikao kazi kilichoitishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Fatuma Omari Latu.
No comments:
Post a Comment