Saturday, April 27, 2019

SUBIRA MGALU AKAGUA VIKUNDI CHALINZE.

 Kina mama wa kikundi cha "NAMNYAKI" kilichopo kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze wakimvisha vizuri mkufu, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea vikundi vilivyokopeshwa na Halmashauri ya Chalinze, Mkufu huo ambao mara nyingi huvaliwa na jamii ya kimasai alipewa zawadi na vikundi vya kata ya Pera katika Halmashauri hiyo.
 
 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, akivishwa Mkufu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) kata ya Pera Tatu Bakari Mpogo, Mkufu huo umepewa zawadi kutoka kwa kina mama wa kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze alipokuwa katika ziara ya kutembelea vikundi vilivyokopeshwa na Halmashauri hiyo.
........................................ 


Halmashauri ya Chalinze ambayo imeanzishwa mwaka 2015, imeshakopesha milioni 900 kwa vikundi mbalimbali vya wanawake vijana na walemavu kwaajili ya kujiendeleza katika shughuli za kiuchumi.


Hayo yamebainishwa jana Aprili 26, 2019 na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu alipokuwa kwenye ziara katika Halmashauri hiyo kukagua vikundi vilivyopata mikopo ili kujua maendeleo ya vikundi hivyo.


Subira mgalu ambae ni miongoni mwa wanaopitisha mipango ya Halmashauri hiyo kupitia Baraza la Madiwani alisema ni wajibu wake kupitia vikundi hivyo ili kujiridhisha kama fedha zilizotolewa zimeleta mafanikio au la.


Katika ziara hiyo ameweza kutembelea kata nane za Halmashauri ya Chalinze ambapo amejionea vikundi mbalimbali vilivyokopeshwa na kurejesha kwa wakati.


Baadhi ya kata hizo ambazo vikundi vyake vimepewa miokpo ni pamoja na Bwilingu milioni 88, Msata milioni 70 huku kata ya Msoga ikiwa imepata milioni 49.5 kwaajili ya vikundi vyake.


Mgalu alisema kupitia Halmashauri ya Chalinze vikundi vinaweza kujikwamua kiuchumi kwa kukopeshwa fedha kwaajili kujiendeleza kiuchumi.


Alisema serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Magufuli inatambua changamoto wanazopata wananchi kiuchumi ndiomana imeamua kutoa mikopo isiyokuwa na riba ili kuwainua kiuchumi kupitia vikundi vyao.


Wakati huo huo Mgalu ametoa ahadi ya kutafuta walimu wa kufundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali ili kuwaongezea ujuzi katika maswala ya kujiongezea kipato.


Aliongeza kwa kusema kuwa, Halmashauri ya Chalinze imekuwa ya kwanza katika ukopeshaji ndani ya mkoa wa Pwani wenye Halmashauri tisa.


Alisema kufuatia hali hiyo, Halmashauri ya Chalinze imeshika nafasi ya kumi kitaifa kati ya Halmshauri 185 zailizopo nchini.


Wakielezea mafanikio waliyopata kupitia mikopo hiyo wanavikundi hao wamesema mikopo hiyo imewainua kiuchumi hali iliyopelekea baadhi ya vikundi kununua magari huku vikundi vikiwa tayari vimemudu kujiendesha bila ya kukopa tena na badala yake wanajikopesha wenyewe ndani ya vikundi kutokana na akiba walizonazo.


Jailani Hafidhi ni katibu wa kikundi cha Walemavu Tunaweza Chalinze (TUCHA) kilichopo kata ya Lugoba amesema kikundi cha wamekopeshwa milioni tatu na kwamba fedha hizo zimewawezesha kuendesha biashara utengenezaji wa maua na kuyauza.


Jailani alisema anaipongeza Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Rais Magufuli kwa kuwajali walemavu ili nao waweze kufanya shughuliza kujiongezea kipato kupitia mikopo hiyo.


Aidha, alisema katika hali isiyo ya kawaida Rais Dkt. Magufuli ameonyesha kuwajali walemavu kwa kuwapa nafasi mbali mbali wizarani jambo ambalo limewapa faraja walemavu.


Nae katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, Getrude Boniface Sinyiza, amesema wananchi waache kudanganywa na watu wanaodai kuwa watawapa mikopo kwa kulipa gharama kidogo na badala yake waunde vikundi ili wapate mikopo inayotolewa na serikali bila ya kutoa kiasi cha fedha.


Alisema mikopo ya serikali inatolewa kwa kukidhi vigezo kupitia vikundi na sio kwa kutoa fedha kama usajili hivyo wananchi wakaacha mikopo yenye mashaka ili kuepuka usumbufu.

katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, Getrude Boniface Sinyiza, akizungumza na wanavikundi katika Halmashauri ya Chalinze wakati wa ziara ya Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, (aliyekaa chini katikati) iliyolenga kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bagamoyo, Rukia Masenga.

Kushoto ni katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, Getrude Boniface Sinyiza, katikati ni Katibu msaidizi wa UWT Mkoa wa Pwani, na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya utafiti ya UWT Mkoa wa Pwani, Salama Shaibu, ambao waliungana na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalu katika ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauriya Chalinze
    Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze, Tatu Bakari Mpogo, (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kikapu Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, wakati alipofanya ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo.

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, akizungumza na wana vikundi kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze.


 
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu,akijaribu Gari ambalo limenunuliwa na kikundi cha Amani kilichopo kata ya Bwilingu.


 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, akifurahia jambo na wana vikundi Chalinze, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bagamoyo, Rukia Masenga.

 Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu, (kulia) akiangalia maua yanayotengenezwa na kikundi cha Walemavu Tunaweza Chalinze (TUCHA) kilichopo kata ya Lugoba, katikati ni Katibu wa kikundi hicho, Mwalimu Jailani Hafidhi, na Kushoto ni Diwani wa kata hiyo Rehema Mwene.
 
Baadhi ya viongozi wa vikundi wa kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu wakati alipofanya ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa vikundi wa kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mh. Subira Hamisi Mgalu wakati alipofanya ziara ya kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri hiyo.

No comments:

Post a Comment