Tuesday, April 30, 2019

RIDHIWANI APONGEZWA CHALINZE KWA KUTEKELEZA AHADI.


Na Shushu Joel, Chalice.

MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amekuwa gumzo jimboni humo mara baada ya kutimiza moja ya ndoto zake alizokuwa akizifikilia kuwatimizia wananchi wake.


Ujasili wake na uthubutu wake katika kuhakikisha wananchi wake wa chalinze wanakuwa na neema ndio umepelekea kuwa Gumzo kila kona ya jimbo la chalinze.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Miono Mbunge wa jimbo hilo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa hakuna kijiji kitakachorukwa na mradi wa Usambazaji umeme vijijini (Rea).


Alisema kuwa wakati anaanza ubunge alikuwa akijiuliza ni lini changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme itamalizika ingawa nilijua kuna siku wananchi wangu wote kuna siku watakuwa nuruni. 


"Umeme ni ajira hivyo ukitumika ipasavyo utapunguza tatizo la ajira kwa vijana na hata kuchangia kwa ongezeko la pato katika Halmashaur yetu kupitia kuanzishwa kwa fursa mbalimbali kwa kupitia upatikanaji wa umeme chalinze.


Alisema kuwa nchi hii kuna wabunge wengi hivyo mwenye kuishawishi serikali anafanikiwa mapema na kufanikisha maendeleo katika eneo lake,lingine ni ukaribu na wadau mbalimbali wenye dhamira chanya ili kufanikisha miradi Aidha alisema kuwa jimbo la chalinze lina jumla ya vijiji 74 na vyenye umeme ni vijiji 34 na vijiji 40 vitakamilika muda si mrefu kwa agizo la serikali ya awamu ya tano.


Mbali na hayo Kikwete amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa juhudi zake anazozifanya katika jimbo hilo kwa kuhakikisha wananchalinze wananufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo.


"Nakumbuka siku unakuja kuomba kura kwa wananchi na kuwaambia utawaletea maendeleo na watashangaa pia uliwataka wananchi kumwagalia Mbunge wa jimbo Lao Ridhiwani Kikwete kwani ni Jembe linalolima usiku na mchana pasipo kusubili mvua"Alisema Ridhiwani .


Kwa upande wake waziri wa nishati Dk Medad Kalemani amempongeza Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kwa utendaji wake wa kazi katika jimbo la chalinze ambalo ni kubwa lakini ni jimbo lenye maendeleo mbalimbali.


Alisema kuwa kutokana na jinsi gani Mbunge huyo anavyomsumbua juu ya suala la umeme ameagiza kuwekwa kwa umeme katika vijiji vyote vya kata ya Miono bila kurukwa kwa nyumba ya aina yeyote ile.


 Aidha waziri huyo amemhakikishia Mbunge huyo kuwa serikali kupitia wizara yake imekubaliana kupeleka umeme katika vijiji vyote vilivyobaki katika jimbo hilo na jambo hilo lianze mara moja. "Serikali ya awamu ya tano iko makini kuhakikisha wananchi wake wanapatiwa huduma zote pasipo kuangalia itikadi ya kisiasa" 


Aidha Dk Kalemani amewataka wakandarasi kote nchi ni kuhakikisha wanawapatia ajira vijana wanaozunguka miradi ili kurahisisha utendaji wa kazi pia kuwapatia fursa vijana wa maeneo husika ambako miradi inapita.


Aliongeza kuwa anatoa onyo kwa wakandarasi wanaochelewesha kuwaunganishia wananchi umeme huku wakiwa wamesha maliza kulipia fedha zao za kuunganishiwa umeme ambazo ni shilingi elfu 27 iwe Rea au Tanesco.

No comments:

Post a Comment