Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Gilles Muroto akionesha Pembe za Ndovu
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 03, 2019 jijini hapa
walizozinasa kutoka kwa askari magereza wa gereza la Msalato A.8070
SSGT Cosmas Ndasi (51)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Gilles Muroto
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 03, 2019 jijini hapa wakati akitoa
taarifa mbalimbali za matukio.
..................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Askari Mageraza wa gereza la Msalato
A.8070 SSGT Cosmas Ndasi (51) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa
tuhuma za kukutwa na pembe za ndovu vipande sita vyenye thamani ya sh
103.5 milioni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma
Gilles Muroto akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa amesema kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa April mosi mwaka huu katika mtaa wa Kilimani
akiwa na vipande hivyo vya pembe vyenye uzito wa kilogramu 13 sawa na tembo
watatu.
“Tulitengeza mtego na Askari huyo
akanasa na kumkamata akiwa ameficha kwenye mfuko vipande vya pembe za
ndovu kwa ajili ya kumsubiri mteja ili kufanya mauzo,” amesema Muroto.
Katika tukio jingine Muroto
amesema kuwa wanamshikilia Ambokile Mwampulo (32) kwa tuhuma za kujifanya
afisa usalama wa Taifa na kudanganya watu ili kujipatia fedha.
Aidha amesema kuwa mtuhumiwa
alikamatwa machi 26,2019 jijini hapa akiwa na nakala za vyeti 15 vya watu
mbalimbali, barua tatu za maombi ya ajira za watu tofauti na nakala ya leseni
moja.
“Kabla ya kukamatwa alijipatia fedha
kiasi cha sh 950,000 kutoka kwa watu wawili ambapo mmoja alimpatia 550,000 na
mwingine alitoa 400,000 lengo ni kupatia ajira. Watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani upelelezi utakapokamilika,” alisema.
Hata hivyo Muroto ametoa wito kwa
wananchi kuwa Serikila ina taratibu na mifumo yake ya kuajiri na si kutumia
watu au vishoka hivyo amewataka kujihadhari na matapeli wa aina yeyote.
Wakati huo huo Muroto amesema
kuwa wanamshikilia Mohamed Hamis kwa tuhuma za kujipatia magari mawili
kwa njia ya udanganyifu.
Kamanda ameyataja magari hayo
kuwa ni Toyota land cruser V-8 lenye namba zausajili T 366 BRX rangi nyeusi na
Toyota aina ya NOAH yenyeno za usaji T 581 DKS ambayo yaliibiwa jijini Dar salaam
mwaka 2017.
“Wakati matukio hayo yanatokea
mtuhumiwa alijitambulisha kwa mwenye magari kuwa ni afisa wa usalama anahitaji
magari kwa ajili ya kazi maalum ambapo aliandika mkataba wa kukodi magari hayo
na alipoyapata alitoweka hadi alipokamatwa,” amesisitiza
Na mtuhumiwa pamoja na magari
hayo atapelekwa jijini Dar es salaam alikoshitakiwa na atafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) Gilles
Muroto, akionesha nakala za vyeti 15 vya watu mbalimbali, barua tatu za maombi
ya ajira za watu tofauti na nakala ya leseni moja ambazo zimekamatwa zikiwa na
mtuhumiwa Ambokile Mwampulo (32) aliyejifanya Afisa usalama wa Taifa na
kudanganya watu ili kujipatia fedha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
leo Aprili 03, 2019 jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog
CHANZO: FULL SHANGWEBLOG.
No comments:
Post a Comment