Na
Hadija Hassan, Lindi
KUFUATIA
kuwepo kwa taadhari ya uwepo wa kimbunga cha Kenneth Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey zambi ametangaza kuahailishwa kwa shughuli zote za Serikali ikiwa
pamoja na Siku ya Malaria Duniani yaliyokuwa yanatarajiwa kufanyika kitaifa
Mkoani Humo April 25, mwaka huu
Mkuu
huyo wa mkoa ameyasema hayo leo April 25, 2019 alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari Ofisini kwake mkoani humo
Maadhimisho
hayo ya Siku ya Malaria Duniani Yalitarajiwa kufanyika Leo katika viwanja
vya Shule ya Msingi Mpili pili Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani
Humo ambapo Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo alitarajiwa kuwa Waziri wa
Afya jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Zambi
amesema kutokana na hali ya taadhari inayoendelea kutolewa na Mamlaka ya
hali ya Hewa hapa Nchini Serikali Mkoani humo kupitia kikao chao cha kamati ya
ulinzi na usalama wameamua kufikia maamuzi hayo
“Jana
tumepata taarifa ya kuwepo na Kimbunga cha aina ya Kenneth ambacho kwa maelezo
ya taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Nchini , inaonyesha
kimbunga hicho kinaelekea katika pwani ya Kusini ya Nchi yetu ambacho
kinatarajiwa kuleta madhara makubwa maeneo ya pwani ya kusini , hasa Mikoa ya
Ruvuma, Mtwara na Lindi inaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa sana Hivyo ni
muhimu kwa wakazi wa Maeneo haya tukachukuwa taadhari za kutosha ”
Kwa
mujibu wa Zambi alisema kimbunga hicho cha Kenneth kinatarajiwa kukumba
Mkoa huo kuanzia saa sita usiku wa Tarehe 25/04/2019 ambacho kinatarajiwa
kuambatana na upepo mkali na Mvua kumbwa
Alisema
kimbunga hicho kinatarajiwa kwenda umbali wa kilomita 60 kutoka ufukweni
mwa bahari sawa na viwanja 600 vya mpira wa Miguu
Zambi
pia aliwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya chini kutoka usawa
wa bahari kuyahama makazi yao kwa kwende maeneo ambayo ni salama
zaidi mpaka pale hali hiyo itakapotulia
Aidha
Zambi aliwataadharisha watu wote wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi
katika pwani hiyo ya Lindi kusitisha shughuli hizo kwa muda pamoja na wale
wanaotaraji kusafiri kwa kutumia njia ya Bahari kusitisha safari zao
Hata
hivyo zambi alisema kutokana na kasi ya kimbunga hicho kutarajiwa kuwa kikubwa
na chenye kasi zaidi pia wameamua pia kusitisha safari zote za Nchi kavu Kwa
Taadhari zaidi mpaka pale watakapotangaziwa kupitia vyombo mbali mbali vya
Matangazo
Zambi alisema licha ya
kughalisha shughuli za Serikali kwa Siku ya Leo halitawahusu watumishi wa idara
za Afya katika zahanati, Hospitari za Rufaha na Wilaya lakini pia taasisi za
kijeshi kama jeshi la polisi na zimamoto na uwokoaji pwmoja na kamati za mahafa
katika maeneo yao kwamba wataendelea kama kawaida
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga alisema kuwa kufuatia
taadhari hiyo tayari kama wilaya imeshatenga maeneo maalumu kwa ajili ya
kujihifadhi kwa muda wananchi ambao watayahama makazi yao kwa ajili ya
kukipisha kimbunga hicho
Ndemanga
aliyataja maeneo hayo kuwa ni Shule ya Msingi Wailesi, Mtanda, Tulieni, Shele
ya Sekondari ya Angaza pamoja na kambi ya Jeshi iliyopo kata ya Mtanda Manispaa
ya Lindi Mkoani humo
Alisema
maandalizi mengine ambayo wameafanya ni pamoja na kuweka utayari kwa boti za
Halmashauri hiyo pamoja na za watu Binafsi kwa kushirikiana na jeshi la
zima moto na uwokoaji kwa ajili ya uwokoaji endapo kimbunga hicho kitatokea
Nae
mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya jinsia wazee na Watoto Dr Leonard
Subi aliwataka wananchi kuendelea kuchukuwa taadhari juu ya kimbunga hicho ikiwa
pamoja na kuondoa vitu vinavyoninginia katika nyumba zao , kuepuka kukaa karibu
na Madilisha pamoja na kuwashahuri kutofunga milango ya Nyumba zao ili kuruhusu
upepo kupita huku akiwataka wananchi hao kukaamaeneo salama hasa ndani ya
nyumba wakati wa kimbunga hiko kikitokea
Subi
pia Alieleza ili kuepuka vitu vingine kuwadondokea katika miili yao ni vyema
kwa wananchi hao wakakaa chini ya meza ama uvunguni mwa kitanda ili waweze kuwa
salama kwa wakati huo
“tunajua
kimbungi hiki kinaweza kuwa na Mvua nyingi na uwenda kukatokea hata mafuliko ni
vizuri pia wananchi mkajiandaa kisaikilojia kwamba jambo hilo linaweza
kutokea tunawashauri wananchi mnaweza pia kutumia madumu kwa ajili ya
kujiokoa , na ikitokea hayo mafuliko yakawepo alisema Subi
No comments:
Post a Comment