Msimamizi wa Usalama wa Waandishi wa
Habari wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Patrick Kipangula
akitoa neno la ufunguzi wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali
kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
.......................................
SERIKALI
imesema kwamba iko tayari kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine kuhakikisha usalama wa
waandishi wa habari wakati wakitekeleza kazi zao.
Kauli
hiyo imetolewa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo wakati wa
kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa
habari.
Akizungumza
kwa niaba ya wizara Msimamizi wa Usalama wa Waandishi wa Habari, Patrick
Kipangula alisema kwamba serikali imeweka mazingira sawa ya kumlinda mwandishi
wa habari ili kuiwezesha nchi na wananchi kuwa na taarifa za uhakika zinazogusa
maisha na maendeleo yao.
Alisema
kwamba katika kongamano hilo ni vyema washiriki wake wote wakatazama rasimu
hiyo ambayo itakuja kuwasilishwa katika kikao kikubwa cha kitaifa kuzungumzia
usalama wa waandishi.
Akizungumzia
masuala ya sasa ambapo kukitokea tatizo kuhusu waandishi kunakuwa na malalamiko
mengi, alisema kwamba ni vyema ikatambulika kwamba sehemu nyingi duniani na
hapa nchini matatizo mengi dhidi ya waandishi wa habari hayasababishwi na
serikali bali na watu binafsi.
Alisema
waandishi wanapaswa kuelewa sheria wanazofanyia kazi ili kujua haki zao na pia
kujua misngi ya usalama wao.
Alisema
ni matumaini yake kwamba taarifa hiyo inayopikwa itasaidia kutambua
mazingira ya waandishi hapa nchini na kuwezesha kuwa na usalama zaidi kama
Umoja wa Mataifa unavyotaka katika kuzingatia vipengele vyake vya maendeleo
endelevu hasa kipengele cha 16 na 10 hasa kifungu cha kwanza na cha pili
kinachogusa usalama waandishi wa habari na wafanyakazi wa habari.
Alisema
kwa sasa serikali imepania kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanakuwa
salama na kwamba uhuru wa habari hautishiwi kwa kuwanyima uhuru waandishi wa
habari.
Alisema
sheria ya vyombo vya habari imetengenezwa kumlinda mwandishi wa habari hasa kwa
kuzingatia kwamba waandishi pia wanatakiwa kupelekwa mafunzo na kuwekewa bima.
Katika
mkutano huo ambao wawakilishi wa UNESCO walikuwepo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini,
Tirso Dos Santos aliwataka washiriki kuchangia ripoti hiyo ili iweze kuwa
msingi wa usalama kwa waandishi wa habari.
Alisema
taarifa hiyo ambayo pia imetengenezwa kwa taarifa kutoka katika mashirika ya
kiraia ni muhimu sana katika utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia.
Alisema
amefurahishwa sana na juhudi za serikali za kuandika taarifa hiyo, huku akisema
mchango wa wadau ni muhimu ili kuwa na ripoti iliyokamilika.
Hii
ni mara ya kwanza kwa serikali kuandaa ripoti kwa kusaidiwa na UNESCO kuhusu
usalama wa waandishi wa habari ingawa mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa
yakifanya.
Ripoti
hiyo ya serikali inatarajiwa kuwasilishwa kwa mamlaka za juu na kujadiliwa Juni
mwaka huu, huku taarifa hiyo ikitakiwa kukamilika Mei.
Naye
Ofisa programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege
alisema katika mkutano huo kwamba ripoti hiyo ni mchanganyiko wa ripoti
mbalimbali ikiwamo maswali yaliyoulizwa kwa kupitia mitandao.
Alisema
kwamba taarifa hiyo inatarajiwa kufikishwa Wizara ya Fedha kabla ya kwenda
kwenye mkutano mkubwa wa wadau.
Alisema
kimataifa shauri hilo litakuwa wazi Julai mwaka huu wakati kwa Afrika itakuwa
ni juni nchini Morocco.
Katika
mkutano huo uliofanyika katika ofisi za UNESCO, wadau walikuwa wanaangalia
rasimu ya serikali na usahihi wake kabla ya kwenda kwenye majadiliano katika
jukwaa kubwa la kisiasa baadae mwaka huu.
Kwa
mujibu wa vipengele vya SDG mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa wanatakiwa
kutoa taarifa za hiari kuhusu usalama wa waandishi wa habari na wafanyakazi wa
vyombo vya habari.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos
Santos akizungumza wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu
usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Ofisa programu wa Unesco kitengo cha
Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege akifafanua jambo wakati wa kongamano la
uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari
lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco
jijini Dar es Salaam.
Wadau wa tasnia ya habari wakitoa maoni wakati
wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa
habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Unesco jijini Dar es Salaam.
Wadau wa tasnia ya habari wakiendelea
kujadiliana wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu
usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos
akifafanua jambo wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu
usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment