Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akiwa anasisitiza jambo mara baada ya
kuwapokea wageni mbali mbali kutoka Compasesion na viongozi wa dini ambao
walifika kwa ajili ya zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni wiki ya
kuadhimisha miaka 20 ya shirika hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo wa kushoto wakipanda mti kwa pamoja na
viongozi kutoka shirika la Compasesion pamoa na viongozi wengine wa dini kutoka
KKKT.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kushoto aliyeshika jembe akifukia udongo
katika moja ya shimo baada ya zoezi la upandaji wa miti ambalo lilifanywa kwa
kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na shirika la Compasesion nje kidogo na
eneo la ofisi yake.
.......................................
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
MKUU
wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amekemea na kupiga marufuku kutofanya
kwa shughuli zozote za kijamii na kiuchumi kwa baadhi ya makundi ya
watu ambao wamekuwa na tabia ya kuvamia hifadhi za misitu kwa
kukata miti ovyo hali ambayo inapelekea ukosefu wa kupata mvua,
mmomonyoko wa udongo pamoja na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Agizo
hilo ametoa wakati wa zoezi la upandaji wa miti lililoandaliwa na Taasisi
isiyokuwa ya kiserikali ya (COMPASESION) ikiwa wiki ya sherehe za
kuadhimisha miaka yao 20 kwa lengo la kuboresha mazingira kwa
kupanda miti katika maeneo tofauti ili kusaidia kurudisha uoto wa
asili ambao hapo awali ulikuwa umeanza kupotea.
Aidha
Mkuu huyo alibainisha kwamba kwa sasa katika Wilaya ya kisarawe kwa kipindi cha
kuanzia mwezi machi hadi Aprili mwaka huu wameshafanikiwa kupanda miti elfu 30
katika maeneo mbali mbali ikiwemo hifadhi ya msitu wa
kazimzumbwi,Pugu,pamoja na kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya bweni ya
wasichana.
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika la Compasesion Kanda ya mashariki ambalo
ndio limeratibu zoezi hilo la upandaji wa miti Shifa Mwagisa
alibainisha kuwa lengo lao kubwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
tano katika kuboresha na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwasaidia watoto ambao
wanaishi katika mazingira magumu.
Pia
meneja huyo alibainisha kwamba mikakati yao ni kuendelea kushirikiana bega kwa
began a serikali ya awamu ya tano pamoja na wadau wengine wa maendeleo kwa lengo
la kuhifadhi mazingira yasiweze kufanyiwa uharibifu wowote ikiwemo pamoja na
kuwasaidia watoto ambao wanatoka katika familia ambazo ni masikini.
Naye
Meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya
Kisarawe Nanzia Shedula alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni
wananchi kuharibu mazingira kwa kuchoma miti na kuikata kwa ajili
ya matumizi ya mkaa, huku mchungaji wa kanisa la kiinjili la Dayosisi ya
mashariki na Pwani Jimbo la kusini magharibi (KKKT) hakusita kutoa kilio chake
juu ya ukataji wa miti.
“Lengo
letu kubwa ni kuendelea kuhakikisha kwamba mazingira tunayatunza kwa hali na
mali lakini changamoto kubwa ni baadhi ya wananchi kuvunja sheria na taratibu
kwa kuamua kuchoma miti ovyo pamoja na kukata miti kwa ajili ya matumizi ya
mkaa lakini kwa sasa hali hii tunajitahidi kuweza ulinzi wa kutoka katika
maeneo ya hifadhi zetu ili kudhibiti hali hii,”alisema Nanzia.
SHIRIKA
hilo la Compasesion katika kutimiza miaka yake 20 tangu kuanzishwa
imeweza kuendesha shughuli mbali mbali za kijamii katika Wilaya ya Kisarawe
ambapo imepanda miti zaidi ya 1500 katika maeneo ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,
Hospitali, Kanisa la KKKT, pamoja na hifadhi ya msitu wa Kazimzumbwi.
Meneja
wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Kisarawe Nanzia
Shedula wa kulia akiwa na viongozi wengine wa dini pamoja na shirika la
Compasesion wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya kupanda mti katika hospitali ya
Wilaya ya Kisarawe.
Viongozi
wa dini kutoka KKKT wakiwa na baadhi ya viongozi wengine wa shirika la
Compasesion wakiwa katika picha ya pamoja mara walipomaliza kupanda miti katika
hospotali ya Wilaya ya Kisarawe.
Baadhi
ya viongozi mbali mbali wa shirika la Compasion pamoja na viongozi wengine wa dini
kutoka KKKT wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate
Mwegelo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji wa miti.
(PICHA ZOTE NA VICTOR
MASANGU)
No comments:
Post a Comment