BUNGE
Viti maalum Mkoani Lindi {CCM} Hamida Abdallah Mohamedi, (kushoto) amkimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Jezi pamoja na mpira kwaajili ya timu ya Namungo FC ya wilaya ya Rungwa Mkonai Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Katibu wa Namungo FC, Johanes Bukine {Mustachi} Jezi pamoja na mpira
.............................
Na
Hadija Hassan, Lindi.
BUNGE
Viti maalum Mkoani Lindi {CCM} Hamida Abdallah Mohamedi, ameipatia Klabu ya
Namungo FC ya Ruangwa, Msaada wa Vifaa vya Michezo vitakavyowawezesha kufanyia
Mazoezi.
Vifaa
walivyoyopatiwa ni Jezi Jozi mbili na Mpira mmoja, vyenye thamani ya Tsh, 350,000/-vimekabidhiwa
kwa uongozi wa Mkoa na baadae kwa viongozi wa timu husika.
Mbunge
Hamida akizungumza katika Mapokezi na kukabidhi kwa Vifaa hivyo, kwenye ukumbi
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, alisema kupanda kwa Namungo FC, kumerejesha
furaha ya wananchi wa Lindi katika Medani ya Michezo, kwani kutawafanya
kuziona timu mbalimbali zikiwemo Yanga, Simba, Azam, Mtibwa na nyinginezo.
“Kwa
kuliona hili, mimi binafsi nimeguswa na ninaiunga mkono kwa kuipatia timu
yetu Jezi na Mpira, ambazo zitawasaidia kufanyia mazoezi” Alisema Hamida.
Pia,
alisema ushindi walioupata timu ya Namungo FC ni wa wana-Lindi wote, baada ya
kupotea furaha hiyo, waliyokuwa wakiipata kutoka kwa timu ya Kariakoo FC, kupotea
katika Medani ya Michezo takribani miaka {15} sasa.
Akipokea
msaada huo, Katibu wa Namungo FC, Johanes Bukine {Mustachi} amemshukuru Mbunge
Hamida kwa msaada huo wa Vifaa, huku akiwaomba wadau wengine wa Maendeleo kuiga
mfano wa kiongozi huyo kwa manufaa ya timu yao.
Bukine
alisema Namungo FC ni timu ya wananchi wote wa Mkoa wa Lindi, hivyo ni vema
wakaiunga mkono kwa kuichangia ili iweze kupiga hatua kwa maendeleo ya Soka.
No comments:
Post a Comment