Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani, Catherine
John Katele, akimkabidhi fulana katibu wa chama hicho tawi la Chuo Cha
Maendeleo Wilaya ya Kisarawe, Regina Mpashobirwa, kulia ni Mratibu wa TUGHE
Muharami Juma, katikati ni Mwenyekiti wa Tawi hilo
..............................
Na
Omary Mngindo, Kisarawe
April
24 CHAMA Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani, kimewataka
wanachama wake kuanzisha miradi, itayowawezesha kujiendesha kupitia asilimia
zinazorudishwa katika vyama vyao.
Aidha
wameshauliwa kufungua akaunti benki zitazotumika kwa ajili ya kuingiziwa fedha
hizo, ambazo wanaweza kuzitumia kwa kujikopesha kisha kurejesha kwa faida
kidogo, hatua itayoviwezesha vyama vyao kujitegemea katika mambo mbalimbali.
Ushauri
huo umetolewa na Mwenyekiti wa TUGHE mkoani hapa Catherine Katele,
alipozungumza na wanachama wa chama hicho wilayani Kisarawe, akiwa kwenye ziara
ya siku mbili ya kukutana na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
"Kuna
asilimia yenu 20 katika kila tawi, lakini kama hamna akaunti itakuwa vigumu
kuwekewa, sababu siwezi kuziingiza katika akaunti ya Mwenyekiti, ni jambo la
muhimu kuwa na akaunti ili mnufaike nazo kwa semina na miradi mbalimbali,"
alisema Mwenyekiti huyo.
Akizungumzia
upandishwaji vyeo na maslahi yao, Catherine alisema kwamba, hilo limetokana na
kazi nzuri inayofanywa na Rais Dkt. John Magufuli, ya kuwabaini watumishi hewa,
na kwamba serikali inafanyiakazi, huku akiwataka waandike barua kwa viongozi
wao kukumbushia masuala yao.
Kwa
upande wao Mwambusa Juma ametaka kujua asilimia zao 20 ambazo hawajarudishiwa
muda mrefu, Mwanana Msumi Afisa Tawala ametaka taarifa za vikao ziwafikie
mapema, huku Mratibu wa TUGHE Wilaya Mwarami Juma akiwahimiza kujitokeza kwa
wingi siku ya Mei Mosi ambayo Kimkoa inafanyika wilayani hapa.
Nae Ramadhani
Maguo kwaniaba ya watumishi wanachama wa TUGHE ameelezea kilio cha kutolipwa
malipo ya likizo kwa miaka zaidi ya mitano, hali inayowaweka katika mazingira
magumu wakati wakiwa katika napumziko hayo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanachama
wa chama hicho, Zuberi Pendeza kwanza alimpongeza Mwenyekiti huyo kwa ziara
hiyo, huku akiomba watembelee maeneo ya kazi kwani wanakabiliwa na changamoto
nyingi.
"Kwaniaba ya wenzangu leo ndio tumepata
elimu na faida ya TUGHE, tunakushukuru sana kwa elimu hii, tunawaomba
mtutembelee maeneo ya kazi tunakabilwa na changamoto nyingi," alimalizia
Pendeza.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani, Catherine
John Katele, akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TUGHE wanaofanya kazi katika Chuo cha Maendeleo ya FDC Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani,
Catherine
John Katele, akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TUGHE
wanaofanya kazi katika Chuo cha Maendeleo ya FDC Wilaya ya Kisarawe
Mkoani Pwani.
PICHA ZOTE NA OMARY MNGINDO.
PICHA ZOTE NA OMARY MNGINDO.
No comments:
Post a Comment