Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za
Misitu Tanznaia Prof. Dos Sanatos Silayo amewataka waajiriwa wapya na wazamani
wa TFS watekeleze majukumu yao kadri sheria za nchi na jinsi maadili
yanavyowataka.
“ Niwapongeze watumishi wapya kwa
kupata nafasi ya kufanya kazi nasi lakini nataka kuwasisitizia kuwa suala la
uadilifu na maadili katika utumishi si la mzaha, enendeni mkalitumikie taifa na
kamwe msisubiri kufanya kazi kwa kusukumwa!
“Kila mmoja anatakiwa kufanya kazi
kwa hiari, kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili
kuhakikisha utumishi wa umma unaleta tija iliyokusudiwa, nanyi watumishi wa
zamani tumewaleta katika mafunzo haya ikiwa ni jitiada za kurejesha uadilifu na
maadili miongoni mwenu, ” alisema Prof. Silayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mafunzo ya
muda mfupi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles Magaya
aliyemwakilisha Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo hicho, Dr. Emanuel Shindika
aliipongeza TFS kwa kutambua kuwa ili utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa
kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja
na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia utoaji wa huduma bora, utiii kwa
Serikali, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika
kwa umma, kuheshimu sheria na matumizi sahihi ya taarifa kwa kuwapa nafasi
yakuwafunza watumishi hao.
No comments:
Post a Comment