Mwanasheria wa Wizara ya Afya Zanzibar Amina
Muhammed Jabir akikagua Mkataba wa ununuzi wa CT Scan mpya uliosainiwa leo
April 24, Mashine hiyo itagharimu Dola Laki nane. Picha na Makame Mshenga.
..................................
Na Fatma Kassim, Afya.
WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana
saini Mkataba wa manunuzi wa mashine mpya ya CT scan na kampuni ya Pacific
Diagnostic Ltd ya Dar es Salaam yenye thamani ya dola laki nane.
Mkataba huo umehusisha ununuzi,
uletaji, ufungaji pamoja na utoaji wa mafunzo ya CT scan kwa Watendaji wa
Wizara ya Afya.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt
Jamala Adam Taib amesema kuwa kupatika kwa mashine hiyo mpya ya CT scan ni hatua
kubwa ya mafinikio kwa Zanzibar ambayo itwasaidia wananchi katika kuchunguza
maradhi mbali mbali.
Amesema Serikali imeona ipo haja ya
kununua mashine hiyo mpya kwa sasa kutokana na kuongezeka kwa huduma mbali
mbali za afya zinazotolewa hapa nchini ambazo zinahitaji uchunguzi wa kina na
waharaka katika mahospitali.
Amesema mashine hiyo itakuwa na uwezo
mkubwa wa kiteknolojia ambapo inatoa slide 128 kwa wakati mmoja ukilinganisha
na iliyokuwepo hivi sasa katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo imefikia
miaka 10 hivi sasa.
Alifahamisha Fedha zilizotumika
kununulia mashine hiyo ni za Serikali kwa asilimia mia moja ambapo alisema ni
juhudi kubwa zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein za
kuhakikisha sekta ya Afya inakuwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wanapata huduma
zenye ubora.
Dkt Jamala alisema tangu kuanza kwa
hatua ya kuwepo kwa mashine ya CTscan kwa Hospitali ya Mnazimmoja kumesaidia
kuwepo kwa huduma nyingi ikiwa na pamoja na kuja kwa Madaktari wa kichwa na
Mgongo kutoka nje ya nchi ambapo wanasaidia na madaktari Wazalendo katika
kuwapatia matibabu hapa nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka
Kampuni ya PACIFC DIAGNOSTIC LTD Brian Kamuzoka ameihakikishia Serikali kuwa
mashine ambayo wataileta hapa nchini ya CTscan ni yenye ubora na aina ya
mashine hiyo inatumika Hospitali kubwa duniani kote.
Amesema baada ya kuifunga mashinene
hiyo watakuwa na mkataba maalumu wa kuifanyia mataengenezo pamoja na
kuisimamaia ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi
No comments:
Post a Comment