Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia mtu mmoja [Jina linahifadhiwa] kwa tuhuma za mauaji ya mtoto
aitwaye JUNIOR BAKARI @ SIAME [12] Mwanafunzi Shule ya Msingi Hayanga Darasa la
III na Mkazi wa Hayanga.
Marehemu alitoweka nyumbani kwao
tangu tarehe 09.04.2019 saa 16:00 jioni wakati anatoka masomo ya ziada na ndipo
mtuhumiwa huyo alimteka na kuondoka naye kusikojulikana na baadae mtuhumiwa
alipiga simu kwa baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye BAKARI SIAME akihitaji
kupatiwe fedha Milioni Kumi [Tshs.10,000,000/=] ili aweze kumuachia mtoto huyo
ila alimnyonga shingo na kumuua na kukimbilia Mkoa wa Iringa maeneo ya Ipogolo
ambapo kikosi kazi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kilifika na kumkamata na
kuja nae Mbeya hadi eneo la tukio.
Ambapo tarehe 13.04.2019 saa 23:00
usiku huko Mtaa wa Shinya, Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jijini na Mkoa wa
Mbeya. Mtuhumiwa [Jina linahifadhiwa] aliwapeleka Askari hadi eneo la tukio
alipomnyongea mtoto JUNIOR BAKARI @ SIAME [12] ambapo mwili wake ulikutwa
umetupwa kwenye shamba la mahindi lililopo maeneo ya Mlima Nyoka.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi
unaendelea.
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
Mnamo tarehe 14.04.2019 saa 20:30
usiku huko maeneo ya Ituta, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Barabara kuu ya
Mbeya – Tunduma, Jiji la Mbeya. Gari yenye namba za usajili T.775 BYV aina ya
Toyota Station Wagon ikiendeshwa na dereva MWAMZI TILA [28] Mkazi wa Uyole
ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni askari G.1008 D/C ANANIA JAMES KIWANGA
[36] askari idara ya Upelelezi, Wilaya ya Mbeya mkazi wa FFU Mbeya aliyekuwa
kazini kizuizi cha magari Ituta – Iwambi na kumsababishia kifo.
Mtuhumiwa amekamatwa na gari lipo
kituoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Chanzo cha
ajali ni mwendokasi. Upelelezi unaendelea.
No comments:
Post a Comment