Tuesday, April 16, 2019

MADIWANI CHALINZE WAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.

Image may contain: 7 people, people smiling, people standing and outdoor
 Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, wakikagua miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya Halmashauri hiyo.
..............................


Kamati ya fedha Utawala na Mipango ya halmashauri ya Chalinze jana Aprili 15, 2019 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa robo ya Tatu ya mwaka wa Fedha 2018/2019.


Ziara hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa halmashauri Mheshimwa Saidi Zikatimu na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bi Amina Kiwanuka.


 Katika ziara hiyo wajumbe wameweza kukagua kizuia cha mapato katika kijiji cha Kihangaiko Kata ya Msata ambacho ni suluhisho kwa wote wanaotumia barabara ya Msata Kihangaiko ili kukwepa kulipa ushuru mbalimbali unaotokana na madini ya kokoto,Ujenzi wa jengo la mionzi katika hospitali ya wilaya ya Chalinze iliyopo katika kijiji cha Msoga Kata Msoga, ujenzi wa vyumba sita vya madarasa katika shule ya Sekondari ya Mdaula iliyopo katika Kata ya Bwilingu.


Aidha kamati ya fedha Utawala na Mipango iliweza pia kukagua ujenzi wa ofisi ya halmashauri inayojengwa katika Mamlaka Ya Mji Mdogo Chalinze kitongoji cha Bwilingu. 


Katika Ukaguzi wa ujenzi huo unaotekelezwa na wakala wa majengo Tanzania, wajumbe wa kamati hawakufurahishwa na hali ya ujenzi wa ofisi hiyo kwani wakala wa majengo wako nyuma ya wakati ukilinganisha na makubaliano kwa mujibu wa mkataba.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Bi Amina Kiwanuka aliwaomba wajumbe wa kamati ya fedha na Utawala kuvuta subira kwani menejimenti ya halmashauri ya Chalinze itakaa hivi karibuni na kuleta mapendekezo katika vikao vya Madiwani na hatua za kuchukua kwa mujibu wa sheria za mkataba na hatimaye kufikia maamuzi ya pamoja kama halmashauri.


Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Mhe Saidi Zikatimu aliwataka wataalamu kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili baraza lake la Madiwani waweze kulijadili suala hilo na kufikia uamuzi ulio sahihi kwa maslahi ya halmashauri na wananchi kwa ujumla.
Image may contain: sky, house, cloud and outdoor
 Image may contain: one or more people, people standing, cloud, sky, house and outdoor
Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, wakikagua miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya Halmashauri hiyo.
 Image may contain: one or more people, shoes and outdoor 
Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, wakikagua miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya Halmashauri hiyo, ambapo hili ni jengo la ofisi za Halmashauri hiyo ambalo linaendelea kujengwa.

No comments:

Post a Comment