NA
HADIJA HASSAN, LINDI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa
(TAKUKURU)Mkoa wa Lindi imemshauri msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Hospitali ya
Wilaya ya Lindi Mkoani Humo kuwataka wasambazaji wa vifaa kuongeza ubora
wa vifaa vya ujenzi huo ama Halmashauri kutafuta wasambazaji wengine wa
Hayo
yamesemwa na kamanda wa TAKUKURU Mkoani humo Stephen Chami mwishoni mwa wiki
iliyopita alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake
lengo likiwa kutoa Taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha miezi
mitatu ' januari hadi machi 2019
Chami
alisema katika kipindi hicho Taasisi yao imefuatilia matumizi ya fedha za
miradi ya maendeleo mbalimbali inayoendelea katika Mkoa huo yenye thamani ya
Tsh. Bilioni 8,180,718,289 ambapo ufuatiliaji huo umefanyika ili kutanzama na
kujilidhisha na miradi husika pamoja na kuona thamani ya fedha zilizotumika
katika miradi hiyo
Chami
aliongeza ushauri huo umekuja baada ya Ya Taasisi hiyo kufanya ufuatiliaji
katika mradi huo na kubaini kuwa kunabaadhi ya vifaa vinavyotumika katika mradi
wa ujenzi wa Hospitali hiyo vina ubora mdogo
Mradi
huo wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Lindi unajengwa katika eneo la
Kiwalala ambapo mpaka kukamilika kwake utaghalimu kiasi cha Tsh. Bilioni
1,500,000,000 ukiwa unasimamiwa na Halmashauri husika kwa kutumia mfumo wa
Force Accout
Pia
Chami pia alisema kuwa Taasisi yao bado inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kila
hatua ya ujenzi huo mpaka utakapokamilika kwa asilimia 100%
No comments:
Post a Comment