Mtu
asiyejulikana amemuiba mtoto wa miezi mitatu aitwae Swaum Saidi na kutoweka nae
kusikojulikana.
Akitoa
Taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, (ACP) Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo limetokea Tarehe
25 agosti 2019 majira ya saa saba mchana maeneo ya Msongola wilaya ya kipolisi
Mlandizi.
Alisema
mama wa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Mariam Shomari mwenye umri wa
miaka 25 aligundua kuibiwa mtoto wake baada ya kurejea nyumbani kutoka kuomba
kibiriti nyumba ya jirani.
Kamanda
Nyigesa aliendelea kusema kuwa, mama wa mtoto huyo alienda kuomba Kibiriti kwa
jirani yake umbali wa mita mia mbili na kwamba baada ya kurejea nyumbani
hakumkuta mtoto wake ambae alimuacha chumbaani.
Alisema
mwizi huyo wa mtoto alitumia mbinu ya kumdanganya mtoto mdogo wa miaka mitatu3,
Fatma Saidi aliyebaki na mtoto huyo kwa kumwambia ametumwa kumchukua mtoto ili
ampeleke kwa mama yake.
Mwizi
huyo wa mtoto alifanikiwa kutekeleza kitendo hicho kiovu cha kuiba mtoto na
kutokomea kusikojulikana.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na msako mkali wa kumtafuta mwizi huyo wa
mtoto.
Kamanda
wa Mkoa wa Pwani, anatoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa, watendaji wa
kata, wenyeviti wa vitongoji na vijiji na wananchi wote kwa ujumla, kutoa taarifa
iwapo watamtilia mashaka mtu watakaemuona na mtoto ili akamatwe.
No comments:
Post a Comment