Thursday, August 1, 2019

MWENGE WA UHURU 2019 WAZINDUA HOSPITALI MSOGA.

 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali, akiwa pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya kikwete, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa halmashauri ya wilaya Chalinze kwaajili ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ya hospitali ya Msoga kuwa na hadhi ya wilaya.
Image may contain: 12 people, people standing 
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, kushoto kwake ni Naibu waziri wa Nishati ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu, kutoka kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis (Bolizozo) Katibu wa CCM wilaya, Salum Mtelela, na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashidi Sharifu, wakisubiri kupokea Mwenge katika hospitali ya Msoga.
 
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali, akisalimiana na mbunge wa kuteuliwa mama Salma Kikwete.
.........................................  

NA MWAMVUA MWINYI,MSOGA

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ameimwagia sifa wizara ya afya kutokana na kuboresha sekta ya hiyo pamoja na kupandisha hadhi kituo cha afya Msoga kuwa hospital ya wilaya.


Akizungumza baada ya mwenge wa uhuru kuzindua huduma za upasuaji katika hospital ya wilaya iliyopo kata ya Msoga halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alisema hospital hiyo ilianza kama zahanati hivyo anashukuru kuongezwa hadhi.


Kikwete alieleza, jitihada za kuimarisha sekta ya afya zinazofanywa na serikali chini ya wizara hiyo zinahitaji kupewa pongezi.


"Mimi ni mzaliwa wa Msoga, kitovu changu kilidondokea hapa, nimefarijika kituo hiki kupandishwa hadhi nina imani itakuwa mkombozi kwa wananchi wa Msoga na maeneo jirani kupata huduma ya matibabu ya karibu na kuondokana na kero ya kufuata huduma umbali mrefu, "alisema Kikwete.


Awali mganga mfawidhi hospital ya Msoga ,Daktari Nelson Luoga alisema, hospital hiyo ilianza kutoa huduma za tiba kama zahanati tangu mwaka 1943 .


"Ilipandishwa hadhi kuwa kituo cha afya mwaka 2016 baada ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete kujenga majengo mapya ndani ya eneo la zahanati ya Msoga."alifafanua Luoga.


Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali, alizindua mradi huo na kusema, serikali inaendelea kuboresha sekta ya afya ili kutoa huduma bora kwa jamii.


Wakati huo huo mwenge huo ulizindua mradi wa josho la mifugo na mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji (lambo), ambapo mke wa Rais mstaafu ambae pia ni mbunge wa kuteuliwa mama Salma Kikwete aliwataka wakulima na wafugaji kuwa kitu kimoja na kuepukana na migogoro baina yao.


Alisema ,washirikiane na kuheshimiana badala ya kuingiliana katika shughuli zao.Awali akipokea mwenge wa uhuru kutoka halmashauri ya Kibaha,mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Kawawa alisema ,mwenge huo umepitia miradi 15 yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 945.1.


Mwenge wa uhuru ulipokelewa mkoani Pwani Julai 24 na kukimbizwa kwenye wilaya saba ,halmashauri Tisa ambapo miradi 95 imepitiwa yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 40.436.6:', kati ya miradi hiyo miradi 61 imekaguliwa,17 ilipaswa kuwekwa jiwe la msingi,9 kuzinduliwa na 8 kufunguliwa huku agost 2 ukitarajiwa kupokelewa mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment