NA
HADIJA HASSAN, MTWARA.
WAZIRI
wa Madini Dotto Biteko amewataka wananchi kulinda rasilimali ya Madini hapa
Nchini ikiwa ni pamoja na kutumia utajili wa Madini uliopo kubadilisha Maisha
yao.
WAZIRI
Biteko ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na Wananchi wa Kijiji cha Pachani
Kata ya Michiga Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu Mkoani Mtwara kuhusu kusitishwa
kwa Shughuli ya uchimbaji wa Madini ya Chuma iliyokuwa inaendea Kijiji hapo.
Biteko
alisema kuwa kwa miaka mingi utajili wa Madini yaliyopo Nchini yalikuwa
yakiwanufaisha wageni huku wenyeji wakiwa bado wanabaki masikini licha ya rasilimali
hizo kuwepo kwenye maeneo yao
“Tanzania
ni tajili Duniani kwa Madini, hata kwa Afrika mzima sisi ni wanne kwa madini ya
dhahabu, wapili kwa madini ya vinto, tunayo Madini mengine mengi ambayo
hayapatikani mahali pengine isipokuwa Tanzania nayo ni Tanzanite” alieleza
Waziri Biteko
“haiwezekani
tunautajili huo halafu watu wetu bado ni masikini ndio maana Rais wetu mnamsikia
kila wakati anasema Tanzania sio masikini,
unaweza
ukasema kuwa masikini kama uwezo wako wa kufikili hujautumia sawasawa”
aliongeza Biteko.
Alisema
uwepo wa Madini hayo na madini mengine yanayopatikana Nchini lazima yawe chachu
ya kubadilisha Maisha ya Wananchi Hata hivyo waziri Biteko aliongeza kuwa lengo
la Serikali la kubadilisha Sheria ya Madini moja wapo ni kutaka kuona rasilimali
hiyo inawanufaisha Watanzania
No comments:
Post a Comment