Askari
wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani wamepata Mafunzo kutoka kwa
wataalam wa Chama cha Madereva Wasafirishaji wa Nchi za nje (ITDA).
Awali
akifungua mafunzo hayo Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani,
Mrakiibu wa Polisi (SP) Mosi B. Ndozero, alisema amefurahi kuona Mkoa wa Pwani
umekuwa ni moja ya Mikoa ambayo imepatiwa Elimu hiyo ambayo itawasaidia Askari
wa usalama Barabarani kuweza kumtambua Dereva anayeendesha gari husika na
uelekeo wa gari hilo katika Nchi jirani.
Kwa upande wake afisa kutoka Chama cha Madereva Wasafirishaji wa Nchi za nje (ITDA), Solomon Kassa alisema mfumo huo utaongeza ufanisi katika kazi na uhakika katika kazi kwa ujumla kwa askari wa usalama barabarani ikiwemo kupunguza ajali za Barabarani zianazosababishwa na madereva (IN-TRANSIT VEHICLES) wasio na sifa Barabarani kwani kwa kutumia mfumo huu madereva wenye sifa ndio watakaoruhusiwa kuendesha magari ya IT.
Sambamba na hilo ameleeza kuwa Chama cha Madereva Wasafirishaji wa Nchi za nje (ITDA) kimedhamiria kuondoa vikwazo visivyo vya forodha ambavyo vipo Barabarani.
Aidha, askari wa usalama Barabarani Mkoa wa Pwani walishukuru maofisa kutoka Chama cha Madereva Wasafirishaji wa Nchi za nje (ITDA) kwa elimu waliyowapatia nakuahidi kwenda kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameyapata toka kwa maofisa hao wa ITDA .
Jumla ya askari walioshiriki walikuwa 44, wawakilishi kutoka kila wilaya za Mkoa wa Pwani wakiwa ni watano, pamoja na ofisi ya RTO Pwani ambao wametakiwa kwenda kuwa mabalozi kwa wenzao kwa elimu waliyopata.
Mara baada ya askari hao kumaliza mafunzo hayo walienda Barabarani kufanya mazoezi kwa vitendo kwa kutumia mfumo wa kielectronic ambapo magari matano ya mfano yalibandikwa Bima ambayo namba ya gari kupitia taarifa ya Bima iliyobandikwa na Afisa wa ITDA inasomwa moja kwa moja kwenye system ya Google ( www.ITDA.co.tz//sticker_verification.php) kwa kumtambua dereva na maelezo yote ya gari anayoendesha na nchi anayokwenda.
Aidha, magari mengi ya IT yanayopita yaliweza kubainika yamebandikwa Bima feki toka Kariakoo kwa mawakala wa Clearing & Forwarding (C&F) kinyume cha utaratibu.
Elimu hiyo iliyotolewa kwa madereva itasaidia kubadilisha mfumo wa kimazoea wa magari ya IT kwenda mfumo wa teknolojia maridhawa kiasi ambacho dereva akifanya kosa/ajali nchini akielekea nchi yoyote ni rahisi kupatikana.

No comments:
Post a Comment