Hadija
Hassan, Lindi.
Ili
kuendelea kupata protini inayotokana na Dagaa wanaotoka kwenye mito, maziwa na
bahari Chuo kikuu cha Dar es saalam kupitia kitengo cha Utafiti wa Vyakula vya
Samaki Kimeanzisha Njia raisi ya kufuga samaki kwa kutumia vyakula vilivyopo
katika maeneo husika.
Hayo
yameelezwa jana na Mtafiti wa Vyakula vya Samaki Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es
saalam Dkt. ,Shadrack Ulomi, alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG
katika viwanja vya Maonyesho ya Wakulima, wafugaji na wavuvi kanda ya Kusini
(nane nane) Ngongo manispaa ya Lindi.
Alisema
kwa kuzingatia umuhimu wa Protini kwa kiumbe kilicho hai katika ukuwaji samaki
kama viumbe wengine na wao wanaitaji protini ya kutosha ili waweze kukuwa
vizuri.
Ulomi
alisema kwa kutumia wadudu na mimea iliyopo katika maeneo husika wafugaji wa
Samaki wataweza kupata vyakula vizuri na vyenye ubora vya kuongeza Protini
kwenye samaki wanaowazalisha
“bidhaa
ambazo tumewaletea wafugaji hapa ni poamoja na njia raisi ya kufuga samaki kwa
kutumia vyakula ambavyo tunaweza tukavitengeneza tukiwa nyumbani ambapo
tumeamua kufanya hivyo Endapo Dagaa watakapokwisha kwenye Maziwa na Mito
angalau watu waendelee kupata protini za kwenye Dagaa kwa kutumia njia Mbadala
kupitia samaki wanaowafuga”
Ulomi
aliongeza kuwa kwa kutumia mimea jamii ya Zola ambayo inakiwango cha protini
kwa 20%-25%, mimea ya lusina ambayo ina protini zaidi ya 25% -30%, wadudu aina
ya Mende wenye Protini 67%-70% wafugaji wa Samaki wanaweza kutengeneza chakula
cha Samaki ambacho ni cha bei nafuu.
No comments:
Post a Comment