Jeshi
la Polisi Mkoa wa Pwani, limemkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Dismas
Siyvester mwenye umri wa miaka 35, kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka mitatu 3,
jina linahifadhiwa.
Akitoa
Taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, (ACP) Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo limetokea Tarehe
19, agosti 2019 majira ya saa tisa alasiri huko Mlandizi "A" kata ya
Mlandizi tarafa ya Mlandizi wilaya ya Kipolisi Mlandizi mkoani humo.
Alisema
mtuhumiwa aliiba mtoto huyo na kwenda nae vichakani kisha kumfanyia kitendo cha
ubakaji.
Aidha,
aliongeza kuwa, mara baada ya taarifa kutolewa, jeshi la polisi kwa kushirikiana
na raia wema lilimkamata mtuhumiwa akiwa na mtoto huyo (aliyebakwa) katika
mashamba ya mboga mboga Vichakani, na kwamba mara baada ya uchunguzi imebainika
kuwa, mtoto huyo ameingiliwa kimwili.
No comments:
Post a Comment