Monday, August 5, 2019

NMB LINDI KUKOPESHA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI.

Hadija Omary, Lindi.

Benki ya NMB Mkoani Lindi imesema itaendelea kushirikiana moja kwa moja na Vikundi vya wakulima, Wavuvi na wafugaji wa Mkoa huo kuwapa mikopo ili kuweza kukuza shughuli zao wanazo zifanya.


Ahadi hiyo imetolewa jana na ofisa wa Benki hiyo Merina Msinza alipokuwa anatoa maelezo juu ya shughuli wanazozifanya mbele ya Mgeni wa Zamu wa maonyesho ya Wakulima (Nane Nane), yanayofanyika Ngongo Manispaa ya Lindi, Sebastian Waryoba.


Msinza alisema katika kuunga jitiada za Serikali za kuinua Uchumi wa jamii ya Watanzania, Benki hiyo imeendelea na itaendelea kutoa mikopo kwa wakulima kama pembejea, matrekta pamoja na pesa Taslimu.


Alisema kwa mwaka wa fedha uliopita zaidi ya Tsh. Miloni 30 Zilikopeshwa kwa vikundi Mbali mbali vya Wavuvi wa Mkoa wa Lindi kwa Wilaya za Kilwa,Lindi Mjini,pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Huku akieleza kuwa pia Benki hiyo imejikita katika utoaji wa pembejeo kwa wakulima wa Korosho pamoja na matrecta ambayo wanayakopesha katika vikundi vya wakulima pamoja na vyama vya Ushirika katika Mkoa huo.


Hata hivyo akizungumza katika Banda hilo La (NMB) katika Maonyesho hayo, Mkuu wa Wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryoba Ameushauri uongozi wa Benki hiyo kufanya Mawasiliano ya Ukaribu na Banki ya maendeleo ya kilimo (TADB) kwa ajili ya Dhamana ya Tahadhari kwa Mikopo inayochukuliwa na wakulima.


Alisema kwa kushirikiana na Benki hiyo ya (TADB) katika utowaji wa Mikopo na kuwadhamini wakulima wao inaweza kuwasaidi namna bora ya kurudisha Fedha Zao za Mikopo zilizokopwa na Wakulima pindi Matatizo yanapotokea.

No comments:

Post a Comment