Na Selemani Magali, Daresalaam.
Kiwanda cha Sayona pamoja na kiwanda cha Elven Agri cha
mapinga Bagamoyo wazalishaji wa chakula asilia cha matunda vimeelezea mikakati yao
ya kulitumia soko la umoja wa Nchi za SADC.
Akizungumza na ujumbe wa SADC uliotembelea viwanda hivyo
hivi karibuni, meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya Elven Agri, Bw Brij Bhayare
amesema sasa wataanza kuangalia soko la nchi hizo ili kukuza biashara yao.
Amesema toka kuzinduliwa kwa Kampuni hiyo na Rais wa awamu
ya Tano, Mh John Pombe Magaufuli mwaka 2017, kampuni hiyo imekuwa ikiuza bidhaa
zake nje ya Mipaka ya Tanzania pamoja na soko la ndani ya Nchi.
“Tumekuwa tunauza bidhaa zetu katika masoko ya Marekani,
Ulaya na Japani, lakini pia tunauza sana katika supermarkets za hapa Tanzania,
tutaangalia pia soko hilo la SADC,” Alisema Brij
Kampuni hiyo kwa sasa inazalisha bidhaa za kusindikwa za
matunda ya maembe, mananasi, na Ndizi mbivu na kwa siku wanapokea tani laki
tatu za matunda.
Amesema wametoa ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi kwa
wakazi wa Mapinga Bagamoyo Tanzania lakini pia kupokea matunda mengi kutoka kwa
wakulima.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Kampuni
ya mitisum group watengenezaji wa vifaa vya ujenzi na vinywaji aina ya sayona
amesema mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi za Jumuiya ya maendeleo kusini mwa
africa (SADC) utatoa fursa ya kuongeza masoko katika nchi hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ,Lugoba Chalinze Mkoani wa Pwani mara baada ya
ziara fupi iliyofanywa na baadhi ya wajumve wa SADC katika kiwanda hicho,
Mlawa alisema kauli ya aerikali ya awamu ya tano ya kujenga viwanda nchini
itakamilika kutokana na mkutano huo utakaofanyika nchini.
Mlawa
alisema ili kusambaza bidhaa zao katika nchi za SADC ,hivi sasa wanejipanga
kujenga soko lingine mkoani Mbeya ili iwe rahisi kwa usambazaji.
Alisema hivi
sasa wanasambaza bidhaa zao katika nchi ya Msumbiiji na Malawi na wanampango wa
kupeleka nchini Ghana.
""Ndio
maana tunasema kuwa mkutano huu utakuwa na fursa kubwa kwa sisi wenyeviwanda
kuweza kusambaza bidhaa zetu kwa urahisi katika nchi za SADC"alisema
Mlawa.
Naye
Mkurugenzi Mratibu wa Kiwanda hicho,Laurance Manyama alisema ,asilimia 95 ya
wafanyakazi ni wazawa na asilimia iliyobaki ni wataalamu kutoka nje ambao
wanawafundisha wazawa.
Manyama
alisema kiwanda chao kinachukua matunda kutoka kwa wakulima nchini zaidi ya
tani laki tatu kwa siku.
Wakati
huohuo,Wakili wa Serikali Godfrey Nyamsanda ,aliueleza uongozi wa kiwanda hicho
kutengeneza bidhaa zilizo na ushindani katika soko la SADC.
"Hii ni
fursa kubwa kwa viwanda vya Tanzania kupata masoko katika nchi za SADC tumieni
fursa hiyo kwa kuzalisha bidhaa zilizo bora"alisema Nyamsanda
No comments:
Post a Comment