Wednesday, August 7, 2019

ULEGA AMUAGIZA MRATIBU WA SWIOFish KUFIKISHA ELIMU YA UFUGAJI WA MAZAO YA BAHARI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega amemuagiza Mratibu wa ‘Mradi wa usimamizi wa uvuvi kusini Magharibi mwa bahari ya hindi (SWIOFish) Flora Luhanga, kufikisha Elimu ya Ufugaji wa Mazao ya Bahari katika Wilaya zote zilizopo katika ukanda wa Bahari ya hindi,



Ulega ameto Wito huo Agosti 06, 2019, katika viwanja vya Ngongo , Manispaa ya Lindi alipotembelea katika Banda la maonyesho ya Nane nane la halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.


Ulega alisema kama mkakati wa Serikali wa kuifanya Nchi kuwa ya uchumi wa viwanda ni wajibu kwa watendaji wa Serikali kuwa wabunifu katika mambo mbali mbali yatakayowawezesha wananchi kukuza vipato vyao.


Alisema Kutokana na uhitaji Mkubwa wa Mazao yanayotokana na Bahari wananchi wanatakiwa kuanzisha ufugaji wa viumbe vya bahari ili waweze kukidhi mahitaji ya soko yaliyopo hivi sasa.


Ulega aliongeza kuwa Baada ya Serikali kufanikiwa kutokomeza Uvuvi Haramu kwa Zaidi ya asilimia 95% hivyo ni wajibu kwa viongozi kutoa elimu inayohusu mazao hayo ya Bahari ili kuwafanya wanachi kutorudia tena uvuvi huo haramu.


Hata hivyo waziri Ulega aliwahakikishia wananchi ambao watajiingiza katika kilimo hicho kuwa na soko la uhakika kwani Serikali imekuwa ikipokea maombi mengi kutoka Nchi mbali mbali kwa Mazao yanayotokana na Bahari kama vile, Jongoo wa Bahari pamoja na samaki kaa (SAGO).


“kama wananchi wanaoishi maeneo ya Bahari watahamasika kufanya ufugaji huu kwa hakika watakuwa na vipato vizuri, mathalani kwa mahitaji ya soko kwa sasa kaa mmoja anauzwa kati ya Tsh, 12,000 hadi 15,000 kwa kilo ambapo ukiangalia ufugaji wake wala hauhitaji gharama kubwa zaidi ya kuzungusha uzio utakaoweza kuingiza maji na kutoka katika eneo la bahari atakalochagua kufugia”


Nae mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Christopha Ngubiagai alisema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakinufaiki na Miradi mbali mbali inayohusu mazao ya Bahari na imekuwa ikifanikiwa kufanya ulinzi katika udhibiti wa Uvuvi haramu kwa kushirikiana na vikundi vya Usimamizi wa Bahari (BMU) vilivyopo katika Wilaya hiyo.


Hata hivyo Ngubiagai aliongeza kuwa Mradi huo wa Ufugaji wa Mazao ya Bahari utaweza kumaliza kabisa Uvuvi haramu pamoja na wanachi kuvua samaki wachanga kwani wananchi watakuwa na kipato cha kutosha hivyo hawatalazimika tena kuvua samaki hao wachanga ama kwa kutumia uvuvi haramu

No comments:

Post a Comment