Na
HADIJA HASSAN, LINDI.
Zaidi
ya asilimia 75% ya Watoto wanaolelewa kwenye mazingira ya upweke, (geti kali)
na wanaokosa vifaa vya kuchezea katika mazingira wanayoishi huchelewa kufikia
hatua za ukuwaji kwa haraka.
Hayo
yameelezwa na Mtaalamu wa Lishe wa Manispaa ya Lindi, Mwenda Gellah alipokuwa
anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG ofisini kwake.
Mwenda
alisema kitendo cha baadhi ya wazazi ama walezi kuwalea watoto wao kwenye
mazingira ya upweke, kunawanyima watoto hao kutofikia hatua za ukuwaji kwa
haraka kutokana na kushindwa kujifunza kutoka kwa watoto wengine.
Alisema
hali ya Mtoto kujichanganya katika michezo na watoto wengine ni namna bora ya
kupata uchangamshi ambao unamuwezesha mtoto kujenga uwezo wake wa kukuwa
kiakili hata kimwili.
Kwa
upande wake Muuguzi mkunga wa Kituo cha Afya mji Manspaa ya Lindi Victoria
Mlope alisema kuwa kitendo hicho cha wazazi kuwafungia Watoto ndani licha ya
kutofikia hatua za ukuwaji kwa haraka lakini pia kitendo hicho kinawafanya
watoto hao kushindwa kupata mahusiano ya kijamii na watoto wenzao.
Hata
hivyo Mlope aliongeza kuwa michezo kwa mtoto humsaidia kuongeza uwezo wa
kujifunza kwa kuujenga ubongo wake ambapo alisisitiza kuwa ni vizuri wazazi
wakatenga muda wa kuwaacha watoto wakachanganyika na watoto wezao katika
michezo mbali mbali ili waweze kujifunza.
Akizungumzia
juu ya Baadhi ya Wazazi/walezi kuwalea Watoto wao kwa geti kali Mkazi wa Manispaa
ya Lindi Othumani Mzee alisema kuwa baadhi ya wazazi wanaowalea watoto wao kwa
namna hiyo mara nyingi wanahofia tabia ovu kutoka kwa watu wanaowazunguka huku
akisema kuwa hiyo ni dhana potofu
“Mtoto
anaweza kuwa na tabia ovu hata asipochangamana na watoto wenzake wa Mtaani
msingi wa kumlea mtoto unatokana na wazai wenyewe kumfungia mtoto sio suluhisho
tunatakiwa kuwafundisha watoto kwa kuwaelewesha lipi zuri na lipi baya bila
hata kuwafungia ndani” alisema Chilewa
No comments:
Post a Comment