Na
Hadija Hassan, Lindi.
Chuo
cha Ufundi Stadi kusini Mashariki (VETA) Tawi la Lindi kimebuni jiko
linalotumia mabaki ya Mkaa (chenga za Mkaa) ambalo linatumia muda mfupi kupika
chakula.
Akizungumza
na BAGAMOYO KWANZA BLOG Mwanafunzi wa fani ya uchomeleaji vyuma Chuo cha veta
Lindi Gerad Miyeye alisema jiko hilo la chenga za Mkaa lina uwezo wa kupika
chakula kwa haraka zaidi kuliko jiko la gesi au Umeme.
Alisema
dhumuni kubwa la kubuni jiko hilo ni kumrahisishia mkulima na Mfugaji katika
kuandaa chakula kwa muda mfupi pindi anapotoka katika shughuli zake za kukuza
uchumi.
Alisema
jiko hilo katika utumiaji wake linatumia boksi feni inayoendeshwa na mfumo wa
umeme wa kawaida au umeme jua ( solar) inayosaidia kukoleza moto kwa haraka.
Nae
mwalimu wa fani ya uungaji vyuma (VETA) Lindi, Lusian Mgila alieleza sababu ya
kubuni jiko hilo kuwa ni baada ya kuona Chenga nyingi za Mkaa zinatupwa baada
ya watu kutumia mkaa ndipo wakaona ipo haja ya kuzifanya chenga hizo ziendelee
kutumika.
Alisema
jiko hilo pamoja na kuwa linapika chakula kwa haraka lakini pia ni rafiki kwa
mazingira kwani inafanya matumizi ya mabaki ya Mkaa kuwa Endelevu
No comments:
Post a Comment