VICTOR
MASANGU, KIBAHA.
KATIKA kuunga mkono azma ya Rais
wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda
serikali Mkoa wa Pwani imejipanga mwezi huu kuweka mawe ya msingi katika
viwanda vipatavyo 13 ambavyo vitajengwa katika Wilaya za Kibaha, Bagamoyo, pamoja na Mkuranga kwa lengo
la kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari
Ofisini kwake wakiwemo baaadhi ya wakuu wa idara Katibu Tawala wa Mkoa wa
Pwani, Bi Theresia Mmbando amebainisha kuwa zoezi hillo la kuweka mawe ya
msingi na kukagua ujenzi wa viwanda hivyo litafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndaikilo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais
Dk. John Pombe Magufuli.
Aidha katika hatua nyingine amekemea
vitendo vya baadhi ya wawekezaji kuwanyanyaza wafanyakazi ambao ni wazawa na
badala yake kuwataka kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote za kazi
na kuwapa vipaumbele zaidi wananchi katika fursa za ajira ili
kutimiza malengo ya serikali katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.
Mkoa wa Pwani katika zoezi hilo
litaweka mawe ya msingi katika baadhi ya viwanda hivyo vikiwemo vya
kiwanda cha kutengenezea mikate na biskuti, kiwanda cha kuzalishia nyuzi, kutengenezea
nondo, sufuria, mitungi ya gesi, kiwanda cha kuchakata mihogo, kamba za uvuvi
pamoja na kingine cha kuchakata zao la korosho pamona na kinachozalisha
chanjo za mifugo.
No comments:
Post a Comment