Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo kulia wakipongezana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Lake
Group Ally Awadhi maara baada ya kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu
tofauti vya kutengenezea nondo,chuma, pamoja na kiwanda cha kutengenezea
mitundi ya gesi katika kata ya visiga Wilayani Kibaha.
.................................
Na Victor Masagu, Kibaha.
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo amewataka wawekezaji wa viwanda kuhakikisha wanazingatia haki za
wafanyakazi kwa kuwalipa maslahi yao kama inavyotakiwa bila la kuwafanyia
vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wowote kwa kuzingatia kanuni, sheria na
taratibu zote za nchi kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya
kuwa na uchumi wa viwanda.
Mhandisi Ndikilo ametoa kauli hiyo
wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya uwekaji wa mawe ya msingi katika viwanda
vitatu tofauti vya kuzalishia nondo, chuma pamoja na mitungi ya
gesi vilivyopo Wilayani Kibaha, ambapo pia hakusita kuwaasa
watumishi na viongozi kuachana na vitendo vya urasimu kwa
wawekezaji na badala yake watoe ushirikiano wa kutosha bila vikwazo vyovyote
kwa lengo la kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi.
“Kwa sasa Mkoa wetu wa Pwani
tunaendelea na kutekeleza agizo la Rais wetu Dk. John Pombe Maguli katika
ujenzi wa viwanda mbali mbali, hivyo kitu kikubwa ninachowaomba wawekezaji wote
wanaokuja kuhakikisha wanazingatia haki za wafanyakazi ili kuweza kutimiza
malengo ambayo yamewekwa na serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025,”alisema Ndikilo.
Aidha katika hatua nyingine
alibainisha kuwa wawekezaji ni chanchu kubwa ya kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo
kwa wananchi kutokana na wengi wao kuweza kupata fursa mbali mbali za ajira
pindi viwanda vinapoanzishwa, hivyo ni jukumu la watendaji na viongozi kuwa
bega kwa bega na wadau wa maendeleo ili kuweza kuongeza zaidi ujenzi wa viwanda
vingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa
makampuni ya lake group Ally Awadhi, alisema, lengo lao kubwa ni kumuunga mkono
Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa viwanda pamoja
na kuwainua wananchi kiuchumi hasa ambao wanaoishi katika kaya ambazo ni
masikini, kuwapatia fursa za ajira.
Pia aliongeza kwamba kutokana na kuwepo
kwa uwekezaji wa viwanda hivyo kutasaidia kuwainua wananchi wa
Wilayani Kibaha pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kutokana na kupata ajira
ambazo zitasaidia kuwaongezea kipato sambamba na kuchangia katika ulipaji wa
kodi amabazo zitafanya pato la Taifa kuongezeka.
Nao baadhi ya wafanyakazi katika
viwanda hivyo walimpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwa na sera ya
ujenzi wa viwanda katika maeneo mbali mbali ambavyo wamedai vimewasaidia
kupata fursa ya ajira, na kuondokana na wimbi la umasikini na kumwomba
mwekezaji huyo kuwaongezea ujira kulingana na kazi wanazozifanya.
Kukamilika kwa viwanda hivyo vitatu
vya utengenezaji wa nondo, na chuma hususan cha kutengenezea mitungi ya
gesi kutaweza kusaidia wananchi kwa kiasi kikubwa fursa za ajira pamoja na
kupunguza changamoto ya ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya kupata nishati
ya mkaa ambayo imekuwa ni kero ya siku nyingi katika maeneo ya Mkoa wa
Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo akiwa anafafanua jambo mara baada ya kumaliza zoezi la kuweka jiwe la
msingi katika kiwanda cha kutengenezea mitungi ya gesi ambacho
kinatarajia kukamilika mwishoni mwa octoba mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama
wa kulia akipeana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni wa Lake Group mara
baada ya kumalizika kwa sherehe za uwekaji wa mawe ya msingi katika viwanda
vitatu.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya
Like group Ally Awadhi kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
wa serikali, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kaati kati
akifuataiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kumaliza
kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu vya kutengenezea Nondo, chuma
pamoja na mitungi ya Gesi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, (kulia) Mhandisi Evarist
Ndikilo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kati
kati, pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Lake group Ally Awadhi
wakipiga makofi kwa pamoja ikiwa ni ishara ya furaja mara baada ya
kukamilika kwa uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalishia
Nondo.
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment