Na
Hadija Hassan, Lindi.
Wawekezaji
wa Sekta ya Madini Nchini wametakiwa kuweka wazi Serikalini makubaliano
wanayowekeana na Wageni wanaoshirikiana nao katika biashara za uchimbaji wa
madini katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea Machimbo ya madini
ya Vinto katika kijiji cha Nditi halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani
Lindi.
Kauli
hiyo ya Biteko imekuja baada ya kubaini uwepo wa ubia baina ya Kampuni ya
Ngwena ya Hapa Nchini inayofanya shughuli ya uchimbaji wa Madini katika Kijiji
hicho cha Nditi na Kampuni ya Indiana ya Nchini Australia ambapo Kampuni ya
Indiana hutoa Fedha kwa ajili ya utafiti wa Madini unaoendelea kijijini Nditi
lakini Kampuni hiyo (Indiana) haionekani popote katika nyaraka zilizopo
Serikalini.
Biteko
alisema ili Serikali iweze kufuatilia kwa karibu na kubaini kinachoendelea
katika Shughuli zote za uchimbaji wa Madini hapa Nchini ni wajibu kwa kila
Mwekezaji katika Sekta hiyo kuweka wazi makubaliano wanayoyafanya na washirika
wao katika Wizara ya Madini.
Aliongeza
kuwa hata katika Sheria ya madini inaeleza wazi kuwa Mtu yeyote aliyepewa
kibali cha uchimbaji hapa Nchini hapaswi kumuingiza muwekezaji wa Nje pasipo
Wizara husika kujua amesema kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
“....wawekezaji
wote wanaojihusisha na uchimbaji wa Madini hapa Nchini ni lazima wajue kwamba
wanapoleta Mgeni kutoka Nje ili kushirikiana nao kwenye Mradi basi lazima kuwe
na uwazi, na kiasi gani cha fedha kinatumika ikiwa ni pamoja na kuonyesha
kwenye mkataba kuwa mradi huo ni wa nani.
La
muhimu kwetu Serikali ni kuona kama makubaliano hayo yanakiuka sheria za Nchi
kama hayakiuki mtaendelea na makubaliano yenu” alifafanua Bitteko Aliongeza
kuwa lengo kubwa la Serikali katika jambo hilo ni kulinda maslahi ya Muwekezaji
mzawa dhidi ya mikataba wanayoingia na Wageni akisema kuwa wajibu wa serikali
ni kuhakikisha muwekezaji mzawa hawezi kunyonywa na mgeni.
Aidha
Waziri Biteko alizidi kusisitiza kwamba serikali haitakubali makubaliano yoyote
yatakayoingiwa na Muwekezaji mgeni na kuruhusu mapato yanayotokana na uchimbaji
huo zaidi ya asilimia 95 yakaenda kwa mgeni.
No comments:
Post a Comment