Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo aliyekaa kwenye pikipiki akiwa na
maafisa taarafa mbali mbali wa mkoa huo pamoja na baadhi ya makatibu Tawala wa
Wilaya mbali mbali katika halfa ya kukabidhi pikipiki 28 kwa maafisa tarafa
iliyofanyika nje ya jengo la ofisi za Mkuu wa Mkoa.
.........................................
VICTOR MASANGU,
PWANI
Serikali
Mkoani Pwani imewaagiza maafisa tarafa wote kutimiza majukumu
yao bila uzembe na badala yake wahakikishe wanashughulikia na kuingilia kati
sakata la wimbi la migogoro ya ardhi ambayo inawakabili kwa kiasi kikubwa
jamii ya wafugaji na wakulima kwani inapelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani na
baadhi ya wananchi kupoteza maisha yao kutokana na kuibuka kwa
mapigano.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati
wa halfa ya kukabidhi pikipiki 28 kwa maafisa taarafa wa Mkoa wa Pwani
zilizotolewa na serikali kuu, ambapo pia amewataka kusimamia na kumaliza
kabisa changamoto ya mimba kwa wanafunzi na kutatua tatizo la kukithiri
utoro.
Aidha
Ndikilo amewataka maafisa hao tarafa kuweka mikakati madhubuti katika
utekelezaji wa majukumu yao hususan katika ufuatiliaji wa miradi mbali mbali ya
maendeleo ili kuwaletea maendeleo chanya wananchi.
“Katika
Mkoa wa Pwani katika baadhi ya maeneo kumekuwepo na changamoto kubwa ya
migogoro ya ardhi kwa hivyo ili suala inatakiwa maafisa tarafa kuifuatilia
wenyewe na kuimalizi sio mpaka viongozi wa ngazi za juu waende kuitafutia
ufumbuzi hivo ninawaomba katika hili tujitahidi kwa hali na mali ili kuondokana
na hali hii ikiwemo suala la mimba kwa wanafunzi na utoro yote myafanyie kazi,”
alisema Ndikilo.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Theresia Mmbando amebainisha kuwa
hapo awali maafisa tarafa walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa
na usafiri wa uhakika hivyo kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati katika
kuwaatumikia wananchi katika suala zima la kuleta maendeleo.
Nao
baadhi ya maafisa tarafa ambao wamenufaika na kupatiwa pikipiki hizo wamesema
kwamba zitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufiuatilia na kusuluhisha kwa
urahisi changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kwani hapo
awali walikuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na
usafiri wa uhakika.
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini, Hamoud Juma, ambaye alihudhuria
katika hafla hiyo, ametoa pongeza za dhati kwa Rais Dk John Pombe Magufuli kwa
kuamua kutoa vitendea kazi hivyo vya usafiri wa pikipiki ambazo zitaweza
kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha ambayo walikuwa wanaipata maafisa
tarafa,
Naye
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mtela Mwampamba alibainisha kuwa ana
imani kuwa changamoto ya awali ambayo walikuwa wanakabiliana nao maafisa hao
itaweza kumalizika kutokana na kupatiwa usafiri huo wa pikipiki ambao utaweza
kuwafikisha katika maeneo mbali mbali ya miradi ya maendeleo pamoja na
kutekekleza kazi zao kwa urahisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimkabidhi pikipiki Afisa tarafa wa
Msoga Juma Mgeni wakati wa halfa iliyofanyika nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini kulia Hamoud
Jumaa akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mtela Mwampamba
mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa maafisa Tarafa wa
Mkoa wa Pwani ambapo pikipiki 28 zimekabidhiwa,
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment