Na
Omary Mngindo, Kibaha.
Mkazi
wa Kijiji cha Soga Kata ya Soga wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Kashinde
Maonaje, amejeruhiwa eneo la shingo kufuatia kupigwa Kareti na muwekezaji Mturuki
akiwa kazini kampuni ya yapiMarkezi.
Mkazi
huyo amepigwa na Mturuki huyo ambaye ni bosi wame, akiwa kazini saa 4 usiku,
baada ya kumkabili kiongozi huyo akimwelezea moja ya changamoto iliyopo,
inayohusiana na utendaji wa kazi anayoifanya kitengo cha umeme.
Alisema
kuwa akiwa katika eneo lake la kazi, kulijitokeza tatizo la kiufundi kuhusu
umeme, ambapo alimfuata bosi huyo akamwelezea hali hiyo, lakini cha kushangaza
alijikuta anapigwa kareti eneo la shingo, hali iliyomsababishia madhara
makubwa.
"Ilikuwa
usiku kulijitokeza tatizo linaohusiana na umeme kwenye kebo, nikamkabili bosi
wangu, ghafla nikamuona amekunja uso, nikajikuta nimepigwa kareti shingoni,
kama mnavyoniona hata kugeuka ni shida," alisema Maonaje.
Baada
ya kujionea tukio hilo baya na la kusikitisha, MNEC Haji alisema kuwa hawezi
kukubaliana na unyanyasaji huo na kueleza kwamba matukio ya aina hiyo yanazidi
kushamiri katika maeneo ya kazi, huku akitaka hatua za kisheria lazima
zichukuliwe.
"Hatuwezi
kuvumilia unyanyasaji aina hii ukiendelea, tunawakaribisha nchini kwetu,
tunawapatia ardhi, mwisho wa siku wanatunyanyasa kiasi hiki, haya ni manyanyaso
yasiyovumilika, kuna maeneo mengine wa-Tanzania wenzetu wanabakwa,"
alisema Haji.
Mbali
ya tukio hilo, Haji aliyeungana na MNEC mwenzake Bundalla Richard kutokea
Shinyanga, alipokea malalamiko kuhusiana na kampuni ya Mohamed Dewj, kupitia
shamba lake lijulikanalo kwa jina la A lave, linalohusiana na kilimo cha
mkonge.
Diwani
wa Kata hiyo Ramadhani Chezeni na wakazi wake walimweleza Haji kwamba, pamoja
na kuwepo kwa usitishaji wa undelezwaji wa eneo hilo, bado kampuni hiyo
inashughulika na upandaji wa mkonge, hali inayowapa sintofahamu kubwa.
"Hili
suala limefika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya na Mkoa lakini mpaka sasa hatuoni
kitu konachoendelea, tunakuomba MNEC lichukue ukamfikishie Mwenyekiti wetu wa
CCM Taifa Rais Dkt. John Magufuli," alisema Chezeni.
Baada
ya taarifa hiyo alimpigia simu mbunge wa jimbo hilo Humoud Jumaa ambaye
alimweleza kwamba suala hilo limefika kwa Waziri nwenye dhamana William Lukuvi,
hivyo anaimani kuwa litakuwa katika hatua mbalimbali.
Kwa
upande wake Haji alimuomba MNEC mwenzake amkumbushe watakapokuwa kwenye kikao
chao mbele ya Mwenyekiti wao Dkt. Magufuli, ili amwelezee kilio hicho
kinachodaiwa kudumu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Haji
aliyekuwa ziarani wilayani Kibaha, alianzia Kata za Gwata na Magindu, ambapo
akiwa Gwata alikutana na mgogoro wa mifugo na mpaka wa vijiji vya Ndwati na
Kigoda, ambapo aliwataka viongozi waumalize, kinyume chake ataufikisha wizarani
ili vifutwe kiwe kimoja kama ilivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment