Na
Omary Mngindo.
Wakazi
wa Kijiji cha Yombo Kata ya Yombo jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanatamani
kubadilishana kopo la korosho na kilo ya unga, ili kujikimu kimaisha.
Hatua
hiyo inatokana na kukabiliwa na hali mbaya kiuchumi, kutokana na kutegemea
kilimo cha korosho na mahindi, huku sekta hiyo ikikabiliwa na changamoto
luluki, iliwemo kuchelewa malipo ya korosho na mifugo mashambani.
Mkazi
Mwajuma Kilakala akiwakilisha wenzake katika mkutano ulioitishwa na Mbunge Dkt.
Shukuru Kawambwa, Kilaka alisema kuwa, kucheleweshwa malipo ya korosho wanaishi
maisha magumu, huku wakitamani kubadilishana korosho na kilo ya unga.
"Mbunge,
tunaomba utupatie ridhaa sisi wakulima kuuza korosho kwa wanunuzi wa binafsi,
msimu wa kuhudumia mikorosho umefika, malipo yetu bado, tunahitaji kununua dawa
za kupulizia, hela hatuna, pia mtu mwenye kilo mbili za korosho lazima apeleke
kwenye gurio?," alihoji Kilakala.
Kwa
upande wake Juma Hemed amelalamikia ardhi ya shule ya secondari ya Miembesaba
ambapo eneo lake linachukuliwa kiholela, huku Sijali Hemed akilalamikia mifugo
katika mashamba.
Akitolea
majibu ya malalamiko hayo, Dkt. Kawambwa alianza kujibu lililohusiana na
korosho ambapo alisema uuzwaji wa korosho hawezi kulitolea taarifa kwani ni
agizo kutoka serikali kuu linalowataka wakulima kupeleka katika maghara ili
zinunuliwe na serikali.
"Kuhusu
mifugo kuchungwa kwenye mashamba amekemea tabia hiyo, huku akiwataka watu
wanaojihusisha na ufugaji kuheshimu mashamba, huku alisema ataliwasilisha kwa
Mkuu wa wilaya ili hatua zichukuliwe," alisema Dkt. Kawambwa.
No comments:
Post a Comment