Na
Omary Mngindo, Mlandizi.
TAASISI
ya Kiislamu ya Masjid Nour ya Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, inahitaji
kiasi cha sh. Mil. 366 kwa ajili ya kujenga shule ya Kiislamu.
Hatua
hiyo inayolenga kuwajengea maadili mema vijana wa kiislamu ili waondokane na
mmomonyoko wa maadili, imeandaliwa na taasisi hiyo ambayo tayari imeshapata
eneo la kujenga shule hiyo katika Kitongoji cha Vikuruti wilayani hapa.
Katibu
wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo Amin Matambo alisema kuwa, wanataraji
kujenga vyumba vinane vya madarasa, nyumba za walimu, ofisi za walimu, msikiti,
vyoo na gari ambavyo thmanai yake ni sh. Mil. 366.
Aliongeza
kwamba katika baraza la Idd ambalo limefanyika katika msikiti huo, mbali ya
Waumini kuhudhuria baraza hilo pia Maimamu kutoka misikiti mbalimbali ndani ya
wilaya ya Kibaha wamehudhuria kisha kutoa maazimio na kwenda kufanyiwa kazi.
"Ujenzi
wa shule mchakato wake umeshaanza kwa kupata eneo litakalojengwa shule hiyo
Kitongoji cha Vikiruti, tumepanga bajeti ya kufanikisha ujenzi huo ambao ni
kiasi cha shilingi milioni 366, tutachangishana waumini pamoja na wadau
mbalimbali," alisema Sheikh Matambo.
Nae
Imamu wa Msikiti wa Mtongani mjini hapa Sheikh, Juma Ngonyani ameunga mkono maazimio ya ujenzi
wa shule hiyo inayolenga kuwajengea watoto wa kiislam maadili mema.
Aidha
Ngonyani ameongeza kwamba kuna kila sababu ya Maimamu kujiunga kwa umoja
kupambana na baadhi ya walimu wa Madrasa wanaozitumia vibaya dufu katika shughuli
za dua za kumswalia (Mtume Muhamad (SAW).
"Haya
maazimio yaliyofikiwa kwenye baraza la Idd yamekuja wakati mwafaka, kwani
kumekuwepo na baadhi ya walimu wa madrasa wamekuwa na tabia ya kugeuza dua za
kumswalia Mtumeu Mhamad (SAW) kama ngoma za kiduku," alimalizia Sheikh
Ngonyani.
No comments:
Post a Comment