
Mwili wa Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Mohammed Dahman, umeswaliwa jana jumanne Agosti 06, 2019 jioni katika Msikiti wa Aboubakar mjini Cologne.
Taarifa zilizoripotiwa na Idhaa ya Kiswahili ya DW, zimesema kuwa, mara baada ya kuswaliwa yanafanyika maandalizi ya mwili huo kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao Zanzibar ambapo unatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi.
Mohammed Dahman, alifariki dunia siku ya Ijumaa (02.08.2019) mjini Cologne, magharibi mwa Ujerumani.
Waumini wa dini ya kiislamu ikiwa ni ndugu, jamaa na marafiki wa Mwandishi, marehemu Mohammed Dahman walipojumuika pamoja kuswali swala ya jeneza ya Mohammed Dahman, jana katika Msikiti wa Aboubakar mjini Cologne, magharibi mwa Ujerumani.
Jeneza
lililobeba mwili wa marehemu Mohammed Dahman likitolewa msikitini mara baada ya
kuswaliwa hapo jana juma nne katika Msikiti wa
Aboubakar mjini Cologne, magharibi
mwa Ujerumani.
Waumini wa dini ya kiislamu ikiwa ni ndugu, jamaa na marafiki wa Mwandishi, marehemu Mohammed Dahman walipojumuika pamoja kuswali swala ya jeneza ya Mohammed Dahman, jana katika Msikiti wa
Aboubakar mjini Cologne, magharibi
mwa Ujerumani.

No comments:
Post a Comment