Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Wizara Maliasili na Utalii kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Brigedia
Generali Mbaraka Mkeremy amewapongeza waahasibu na watumishi wa TFS kwa
kuchagiza TFS kupata Hati Safi za Ukaguzi.
Akizungumza katika kikao na Watumishi
wa Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini jijini Mbeya jana, Brigedia Generali Mkeremy
alisema licha ya TFS kuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yake watendaji wake wameweza kufanya kazi kwa weledi na
hata kufanikiwa kupata hati safi kwa mara ya kwanza.
“Najua taasisi hii ina changamoto
nyingi lakini niwapongeze kwa namna mlivyojituma na hata kuweza kupata hati
safi ya ukaguzi, hati hii ni matokeo ya uwajibikaji katika makusanyo na
matumizi.
Nimeelezwa kuwa TFS pia ilivuka
malengo ya makusanyo, na imefanikiwa kupunguza malalamiko na kutokuwapo
migogoro baina ya watumishi na hayo ni kiashiria cha mafanikio ya taasisi,” Brigedia
Generali Mkeremy alisema.
Hii ni mara ya kwanza kwa Brigedia
Generali Mkeremy kuzungumza na watumishi wa kada tofauti wa TFS tangu Waziri wa
Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla aizindue Bodi ya Ushauri ya Wizara
kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jijini Mwanza na kuhudhuriwa na
wadau mbalimbali Machi 9,2019.
Brigedia Jenerali Mkeremi alisema
kukabiliana na baadhi ya changamoto hususan ujangiri TFS imeamua kuingia kwenye
Jeshi Usu ili kuhakikisha uhifadhi endelevu wa misitu nchini.
Kamishna Mhifadhi wa Misitu, Prof.
Dos Santos Silayo aliwataka watumishi kuendelea kushirikiana katatika kutatua
changamoto za kiutumishi na kiutendaji huku akitanabaisha kuwa mabadiliko ya
Jeshi Usu yataenda sambamba na TFS kutoka kwenye Wakala na kuwa Mamlaka kamili.
No comments:
Post a Comment