Thursday, August 1, 2019

SHULE YA MORDEN CHALINZE YATUMIA MIL. 235 UPANUZI WA SHULE.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Ally Mkongea akijiandaa kukata utepe katika jengo la vyumba vinne vya madarasa kwenye shule ya msingi ya Chalinze Modern Islamic. Picha na Omary Mngindo.

................................
Na Omary Mngindo.

 KIASI cha shilingi milioni 235 zimetumika kwa ujenzi wa shule ya msingi ya Chalinze Modern Islamic, iliyoko Kijiji cha Chalinze Mzee Kata ya Bwilingu wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.


Shule hiyo ya binafsi inayomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji Omari Swedi, inalenga kuunga mkono juhudi za serikali katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini na kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa watoto wa Kitanzania kwenye mazingira rafiki.


Kiasi hicho cha fedha zimetumika kwa ajili ya majengo mawili tofauti, ambapo bweni la wasichana limegharimu shilingi milioni 135,000,000, huku kiasi cha shilingi milioni 100,000,000 zikitumika kwa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa.


Omary Swedi alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 575, kati ya hao 203 ni wakazi maeneo ya Chalinze, sanjali na kuwapatia ajira wakazi na kuchonga barabara inayoelekea kwenye lambo, ambayo pia inatumika na wananchi kwa shughuli mbalimbali.


Alisema kuwa mradi huo unagharimiwa na shule kupitia ada zinazolipwa na wazazi wa wanafunzi shuleni hapo, sanjali na sadaka kutoka kwa watu mbalimbali, huku halmashauri ya Chalinze ikiwasaidia wataalamu katika ufanikishaji wa ujenzi huo.


"Mradi una wanufaisha wanafunzi 575 ambapo kati yao 203 ni wenyeji wa Chalinze, sanjali na kuwapatia ajira wakazi wanaoishi katika maeneo ya Chalinze ambao wamepata ajira, ikiwemo uchongaji wa barabara inayoelekea kwenye lambo la maji.


Akizungumzia ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, Mkurugenzi Swedi alisema kwamba mpaka sasa ujenzi huo upo katika hatua ya umaliziaji, ambapo tayari kiasi cha shilingi milioni 70 zimeshatumika kwenye ujenzi huo.


"Upande wa vyumba hivi vinne vya madarasa vinavyotaraji kutumika sh. Mil. 100, mpaka kufikia hatua hii kukaribia kumalizika tayari zimeshatumika kiasi cha sh. Mil. 70," alisema Swedi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mzee Mkongea Ally katimati akikagua moja ya vyumba vinne vilivyopo katika shule ya Chalinze Modern Islamic iliyoko Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Picha na Omary Mngindo

No comments:

Post a Comment