Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John
Pombe Magufuli leo Agosti 1/2019 amemtengua Bw. Kayombe Masoud Lyoba
aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa
usimamizi usioridhisha wa miradi ya Maendeleo hususani ujenzi wa hospitali ya
Wilaya .
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini
Dar es Salaam, Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI , Suleimani Jafo(MB)
amesema Mkurugenzi huyo alifanya ununuzi wa dawa ya mchwa kwa gharama kubwa ya
milioni 66 kinyume cha gharama halisi.
“kutozingatia taratibu za manunuzi na miongozo ya
matumizi ya fedha za ujenzi wa hospitali za halmashauri ,kufanya ununuzi wa
kokoto kwa gharama ya shilingi Milioni 45 na kuzisafirisha kwa gharama ya
milioni 42” Amesema Jafo
Kufuatia utenguzi huo nafasi hiyo ya ukurugenzi kwa
sasa itakaimiwa na Mhandisi Godfrey George Mlowe amabye ni Meneja wa TARURA
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro hivyo namuelekeza Mhandisi Godfrey Mlowe
kusimamia Halmashauri hiyo pamoja na miradi yote ya maendeleo katika wilaya
hiyo ikiwemo, ukamilishaji wa majengo ya Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Vituo
vya afya vya Mikese na Kinonko vilivyopokea fedha hivi karibuni .
Waziri jafo amesema kuwa ansisitiza ujenzi wa vituo
vya afaya vijengwe kwa utaratibu wa force Account kwa usimamizi wa kamati
zilizoundwa katika ujenzi wa vituo hivyo
Waziri Jafo ameiagiza TAKUKURU iendelee na
uchunguzi wa kina wa michakato yote ya ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilya.
No comments:
Post a Comment