Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari za SADC katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),kuhusu uboreshaji wa miundombinu hasa kwa nchi wanachama wa SADC,Makoena amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuzindua ujenzi wa mradi mkubwa uzalishaji wa umeme mtoto Rufiji,amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki. Picha na Michuzi Jr.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Viwanda katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), ,Calicious Tutalife akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari za SADC katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),Kuhusu uwezeshaji wa biashara huria sambamba na uwepo wa upatikanaji wa ushindani na maendeleo ya Viwanda anuai,kuongezeka kwa uwekezaji wa viwanda na tija,kufuata ubora na viwango vilivyowekwa Kimataifa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC),
Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Viwanda katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC),Calicious Tutalife,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano- SADC Barbara Lopi na Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena .
Wanahabari wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Ujenzi wa mradi wa umeme katika Mto Rufiji umetajwa kuwa wa mfano katika nchi za SADC na nchi wanachama wa Afrika Mashariki wa EAC, kutokana na namna Serikali ilivyoamua kuusimamia.
Akizungumza katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar leo na Wanahabari , Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena amesema mradi huo mkubwa unaojengwa nchini ni wa kipekee, ambao unasimamiwa moja kwa moja na Serikali na unagharamiwa na fedha za ndani.
“Mradi huu mkubwa wa Rufiji ni jambo la kujivunia, sisi SADC tunajivunia na si kwa SADC tu, lakini pia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
Mokoena amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu wake wa kutekeleza mradi huo mkubwa wa umeme, ambao utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi za SADC huku akisema SADC inamuunga mkono katika utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa umeme.
Amesema mradi huo unaonesha unatoa funzo kwamba uongozi unahusika katika kuhakikisha miradi yenye tija inasimamiwa kwa nguvu zote ili kuzinasua nchi zetu katika matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa uwezo wa ndani.
Mokoena amesema kutokana na uhaba wa nishati unaozikabili nchi nyingi wanachama wa SADC, juhudi za ziada zinahitajika kuboresha upatikanaji wa nishati, ambayo ni muhimu katika kutimiza malengo ya uwekzaji katika viwanda na uzalishaji wa bidhaa.
Amesema miongoni mwa mikakati muhimu ya SADC kwa sasa ni kuhakikisha kuwa na uhakika wa nishati rahisi, yenye uhakika, gharama ya chini, kupitia mpango maalumu uliowekewa ukomo wa mwaka 2027.
No comments:
Post a Comment