Na
Omary Mngindo.
Vikundi
vya Ujasiriamali 12 vya vijana, wanawake ndani ya Kata ya Kerege wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani, vimepatiwa mkopo wa shilingi milioni 67 kutoka
halmashauri ya wilaya ya hiyo.
Mikopo
hiyo imetokana na asilimia kumi ya halmashauri hiyo ambayo ni utekelezaji wa
agizo la serikali kwa halmashauri zote nchini kupitia makusanyo yake ya ndani
ya kuvikopesha vikundi mikopo isiyokuwa na riba.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Diwani wa kata ya Kerege, Said Ngatipura
alisema kuwa, vikundi hivyo vimepatiwa fedha hizo kulingana na maombi na kiasi
cha fedha, huku akieleza kwamba vikundi hivyo vinaendelea na marejesho.
"Vikundi
vilivyopatiwa mikopo ni 6 kikiwemo cha Tumaini Kilemela ambacho kimerejesha
vizuri na kukopa tena, katika mikopo hiyo vikundi vya wanawake vimekopeshwa
shilingi milioni 39.5 wakati vijana wakipata mkopo wa shilingi milioni 28
tu," alisema Ngatipura.
Alisema
kuwa Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Mwambao Shumina Sharifu, ametafuta
wafadhili waliowezesha kuchimba visima viwili vya maji safi, kimoja kipo shule
ya msingi Kerege na kingine shule ya Mapinga.
Akizungumzia
sekta ya elimu, Ngatipula alisema kuwa Kata ina shule moja ya sekondari yenye
kidato cha kwanza mpaka cha nne na wanafunzi 1,105, kati yao wavulana 540,
wasichana 565 ikiwa na walimu 75.
Alisema
kuwa mfuko wa jimbo umeunga mkono juhudi za wananchi katika umaliziaji wa
vyumba vya madarasa sekondari ya Kerege, jengo la Utawala, vyoo shule ya msingi
Mapinga, ununuzi wa bati ofisi ya Kitongoji cha Amani na mifuko 100 ujenzi wa
vyumba vya madarasa.
"Pamoja
na hayo, kupitia mfuko wa jimbo umeendelea na utoaji wa ruzuku kwa vikundi vya
ujasiriamali vikiwemo Neema Group, Manofu Woman, Jitambue na Jitahidi ambavyo
vinajihusisha na shughuli za ujasiriamali," alimalizia Ngatipura.
No comments:
Post a Comment