Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akifungua kitambaa katika jiwe la msingi, ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa Usambazaji Umeme
katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban, jana Agosti 06, 2019 katika wilaya ya Bagamoyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban, jana Agosti 06, 2019 katika wilaya ya Bagamoyo.
...................................
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu,amezindua Mradi wa Usambazaji Umeme
katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban Rural Electrification
Program) wilayani Bagamoyo ikiwa ni muendelezo wa uzinduzi wa miradi hiyo nchi
nzima.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Naibu waziri huyo wa Nishati amesema lengo la serikali
ni kuwasha umeme katika vijiji 10,278 ifikapo mwezi Juni 2020, ambapo mpaka
sasa vijiji 7,349 tayari vimeshaunganishwa umeme.
Alisema
katika mradi huo wanachi elfu sita wa awali wataunganishiwa umeme katika maeneo
mbalimbali ikiwemo Kata za Magomeni, Kerege, Zinga, Kiromo Mapinga na vitongoji
vyake katika Halmashauri ya Bagamoyo.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, hayo yote yanatekelezwa kutokana na uongozi mzuri wa Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, kusimamia ukusanyaji wa
kodi ili fedha zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo kama hiyo.
Naibu
waziri huyo wa Nishati ametumia nafasi hiyo kuwaagiza wakandarasi na
wasambazaji na wazalishaji wa vifaa
vinavyotumika kwenye miradi ya umeme kuzalisha vifaa vyenye ubora ili miradi
inayojengwa iwe ya kudumu.
Aidha,
alisema wakandarasi wanapaswa kutumia vifaa vinavyozalishwa na kampuni za ndani
ili kuongeza pato la ndani kutokana na kodi za wenye viwanda hivyo.
Nao
wasambazaji wa vifaa hivyo wametakiwa kuacha urasimu na badala yake wafanye
kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi yao kulingana na mahitaji ya wakandarasi ili vifaa viwafikie wakandarasi kwa
wakati nao waweze kutekeleza miradi ndani ya kipindi cha mikataba yao.
Alitoa
onyo kwa yeyote atakaejaribu kumkwamisha mkandarasi, kuwa hatua hiyo ni
kukwamisha juhudi za wizara, na ukiikwamisha wizara umemkwamisha Rais wa Jamuri
ya Muungano wa Tanzania na kwamba utakuwa ni miongoni mwa wanaorudisha
maendeleo nyuma na serikali haitokuvumilia.
Awali
akizungumza mbele ya Naibu waziri, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) Mhandisi, Amos Maganga, amesema mradi huo utagharimu shilingi Bilioni 12 . 8
utakapokamilika.
Nae
Mbunge jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, amesema anamshukuru Rais Dkt.
Magufuli kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi huo ndani ya jimbo
lake.
Aidha,
amempongeza waziri wa Nishati Medard Kalemani pamoja na Naibu waziri Subira
Mgalu kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusimamia vyema miradi ili itekelezwe ndani
ya wakati.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akikata utepe kama ishara ya kuzindua Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban, jana Agosti 06, 2019 katika wilaya ya Bagamoyo, Kutoka kulia ni Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Dorisi Mwakatobe, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Dailin Leonard Mgweno, kutoka kushoto ni Meneja wa Tanesco Bagamoyo, Daniel Kyando,
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Wakili, Julius Kalolo Bundala, Katibu wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Salum Mtelela, na Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo, Mwanaharusi Jarufu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akitoa maelekezo kwa viongozi wa kampuni ya SINOTEC ambayo ndiyo inayotekeleza mradi huo katikati ni Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Mwakilishi Mkuu nchini Kenya, kutoka Kampuni ya SINOTEC, Jin Hua, wa kwanza kushoto ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara, SINOTEC Tanzania, Xiong Yuezhou.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) Mhandisi, Amos Maganga, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
Madiwani
wakisalimia katika uzinduzi huo, kutoka kulia ni Diwani wa kata ya Fukayosi
ambae pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa, wa katikati
ni Diwani wa kata ya Kiromo, Hassan Usinga (Wembe) na wa kwanza kushoto ni
Diwani wa kata ya Kisutu, Aweso Ramadhani.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, (kulia) na Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo, Mwanaharusi Jarufu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo Bundala, kushoto ni
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,
Kulia ni Kaimu Miurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati
Vijijini, Mhandisi, Amos Maganga, na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Dailin Leonard Mgweno
Meza
kuu, katikati ni Mgeni rasmi, Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, kutoka kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) Mhandisi, Amos Maganga, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Dailin Leonard Mgweno,Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Wakili, Julius Kalolo Bundala, kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Dorisi Mwakatobe, Diwani wa kata ya Magomeni Bagamoyo, Mwanaharusi Jarufu, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,
No comments:
Post a Comment