Kitalu
cha miche bora ya Mikorosho kilichoandaliwa na Taasisi
ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) Naliendele.
Kitalu
cha miche bora ya Mikorosho kilichoandaliwa na Taasisi
ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) Naliendele.
......................................
Na
hadija Omary, Lindi.
Taasisi
ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) Naliendele, Kilichopo Mjini Mtwara imegundua
Njia ya uzalishaji wa Miche ya mikorosho kwa kutumia jani la mti huo.
Hayo
yameelezwa na kaimu Mkumkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Fortunatus Kapinga, jana
katika ufunguzi wa Maonyesho ya Nane Nane kanda ya Kusini yanayofanyika katika
viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi Mkoani humo.
Kapinga
alisema kwa sasa Taasisi hiyo bado wapo kwenye utafiti wa uzalishaji wa miche
ya Mikorosho kwa kutumia majani ya Mti huo ambapo kwa kiasi kikubwa utasaidia
kuzalisha miche mingi kwa wakati mmoja.
Alisema
kwa kutumia njia hiyo jani moja la mti wa Mkorosho linaweza kuzalisha miche 100
ya mti huo hivyo kurahisisha namna bora ya kuandaa miche ya zao hilo.
Hata
hivyo DKT. Kapinga aliongeza kuwa endapo watakamilisha utafiti huo wanaweza
kuongeza uzalishaji wa mashamba mengi ya korosho kwa kupata miche mingi na
mashamba kuongezeka.
"Kwa
sasa bado tunaendelea na utafiti wa kuzalisha miche kwa kutumia jani la mkorosho
na ukikamilika utaongeza thamani ya korosho kuanzia majani, tunda (bibo) na
korosho yenyewe" alisema Dkt Kapinga.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa maonyesho hayo ya Wakulima Nane nae kanda ya Kusini kwa
Niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jaffo Mkuu wa Wilaya
ya Masasi Suleimani Mzee aliipongeza Taasisi hiyo kwa kugundua namna ya
uzalishaji wa Miche hiyo ya mikorosho huku akiwataka watendaji wa Taasisi hiyo
kuendelea kufanya utafuiti katika mazao mengine ili kuongeza tija ya uzalishaji
"Niwapongeze
sana wataalamu wetu wa Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI Naliendele, kwa
kuongeza Wigo katika uzalishaji wa Miche ya Mikorosho kwani wametoka kuzalisha
miche kwa kutumia mbegu ya korosho na sasa wanazalisha miche kwa kutumia jani
la Mti huo hongereni sana” alisema Mzee.
No comments:
Post a Comment