Wananchi
wa Lindi na viunga vyake wakipata huduma za usajili laini za simu kwa alama za
vidole katika banda la TCRA ambapo NIDA na watoa huduma walikuwepo.
...............................
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi
wa Kanda ya Kusini watumie maonesho ya Nane Nane kupata elimu ya Mawasiliano
pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Hayo ameyasema Afisa wa TCRA Abdulrahaman Millas
katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini mkoani Lindi.
Alisema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi
kusajili laini za simu kwa alama za vidole na kwamba huduma zote za kufanya usajili zipo
ndani za maonesho hayo.
Millas aliongeza kuwa, ni vyema kutumia muda
uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole kwani mwisho wa
usajili huo ni Desemba 31 mwaka huu.
Alisema kuwa muda uliopangwa lazima utumike
kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za
Desemba.
“Muda uliowekwa ni mkubwa kwa wananchi kupata
kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho
vya Taifa wasajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa
mawasiliano simu hizo.
Aidha alisema kuwa TCRA ipo bega kwa bega katika
kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalimbali za mawasiliano ili wasitumie
mawasiliano kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment