Pichani
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizingumza na walazi wa Kijiji cha Msigi
(hawapo pichani) wakati Mgalu akiwa katika ziara kwenye Kata za Ubena,
Talawanda na Kiwangwa kukagua vilundi vya Wajadiriamali waliopatiwa gedha
kupitia halmashauri hiyo. Wanaoshuhudia ni Said Mwakapugi ofisa Maendeleo
halmashauri hiyo, Jumanne Rajabu Mwenyekiti wa Kijiji na Said Zikatimu.
Picha
na Omary Mngindo.
...........................................................
Na
Omary Mngindo, Chalinze
WIZARA
ya Nishati imepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 160 kwa ajili ya kufikisha
umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa, kutokana na makosa ya upimaji wa
umbali.
Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameyasema hayo jana akiwa katika ziara ya
kukagua vikundi vilivyokopeshwa pesa za mapato ya ndani ya halmashauri ya
Chalinze mkoani hapa, ambapo aliitumia siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi
kutembelea Kata za Ubena, Talawanda na Kiwangwa.
Akiwa katika vijiji vya Msigi,
Talawanda, Magulumatali na Bago, Mgalu alipokea kilio hicho kutokana kwa
wananchi kuhusu kutofikiwa na umeme, hali waliyoielezea inachangia kudumaza
maendeleo ikiwemo shughuli za kiuchumi, ukizingatia umuhimu wa huduma hiyo.
Akizungumza
na wananchi katika maeneo hayo akiambatana na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Chalinze Said Zikatimu, Mgalu alisema kwamba serikali baada ya kubaini
mapungufu hayo ya kibinadamu, Rais Dkt. John Magufuli alisema hataki
agombanishwe na wananchi, akawapa ridhaa ya kuomba fedha hazina kwa ajili ya
kazi hiyo.
"Mapungufu
yaliyojitokeza, nitolee mfano hapa Magulumatali, waliosimamia zoezia la upimaji
kutokaea Chalinze wamesema kuna umbali wa kilometa 6 wakati uhalisia ni
kilometa 10, pia katika maeneo mengine hivyohivyo, tukaandika ombi hazina
tukapatiwa kiasi hicho," alisema Mgalu.
Aliongeza kwamba zoezi la
usambazaji umeme kwa mradi uliopo wa REA unaendea hivyo wananchi kwa sasa
waendelee na uwekaji wa waya katika nyumba na kwamba umeme utawafikia kama ilivyodhamiliwa
na serikali ya kuwafikishia huduma hiyo wananchi wote.
Nao wakazi wa Kijiji cha
Bago Kata ya Talawanda wamelalamikia kutounganishiwa umeme kwa muda mrefu, huku
huduma hiyo ikiishia kwa majirani zao hali inayosababisha malalamiko mengi kutokana
kwa wakazi hao.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Talawanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu alisema kwamba anaimani na kazi kubwa
inayofamywa na Serikali kupitia Waziri Dkt. Medard Kalemani na Naibu wake Mgalu, kwa
namna wanavyochapakazi, huku akiwaomba wakazi ndani ya halmashauri na jimbo
zima la Chalinze waendelee na uwekaji wa miundombinu hiyo tayari kwa kupokea
huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment