Na
Shushu Joel, Chalice.
MBUNGE
wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amekuwa
gumzo jimboni humo mara baada ya kutimiza moja ya ndoto zake alizokuwa akizifikilia
kuwatimizia wananchi wake.
Ujasili
wake na uthubutu wake katika kuhakikisha wananchi wake wa chalinze wanakuwa na
neema ndio umepelekea kuwa Gumzo kila kona ya jimbo la chalinze.
Akizungumza
na wananchi wa kata ya Miono Mbunge wa jimbo hilo aliwahakikishia wananchi wa
eneo hilo kuwa hakuna kijiji kitakachorukwa na mradi wa Usambazaji umeme vijijini (Rea).
Alisema
kuwa wakati anaanza ubunge alikuwa akijiuliza ni lini changamoto ya upatikanaji
wa nishati ya umeme itamalizika ingawa nilijua kuna siku wananchi wangu wote
kuna siku watakuwa nuruni.
"Umeme ni ajira hivyo ukitumika ipasavyo
utapunguza tatizo la ajira kwa vijana na hata kuchangia kwa ongezeko la pato
katika Halmashaur yetu kupitia kuanzishwa kwa fursa mbalimbali kwa kupitia
upatikanaji wa umeme chalinze.
Alisema
kuwa nchi hii kuna wabunge wengi hivyo mwenye kuishawishi serikali anafanikiwa
mapema na kufanikisha maendeleo katika eneo lake,lingine ni ukaribu na wadau
mbalimbali wenye dhamira chanya ili kufanikisha miradi Aidha alisema kuwa jimbo
la chalinze lina jumla ya vijiji 74 na vyenye umeme ni vijiji 34 na vijiji 40
vitakamilika muda si mrefu kwa agizo la serikali ya awamu ya tano.
Mbali
na hayo Kikwete amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli kwa juhudi zake anazozifanya katika jimbo hilo kwa kuhakikisha
wananchalinze wananufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Nakumbuka
siku unakuja kuomba kura kwa wananchi na kuwaambia utawaletea maendeleo na
watashangaa pia uliwataka wananchi kumwagalia Mbunge wa jimbo Lao Ridhiwani
Kikwete kwani ni Jembe linalolima usiku na mchana pasipo kusubili
mvua"Alisema Ridhiwani .
Kwa
upande wake waziri wa nishati Dk Medad Kalemani amempongeza Mbunge wa jimbo
hilo Ridhiwani Kikwete kwa utendaji wake wa kazi katika jimbo la chalinze
ambalo ni kubwa lakini ni jimbo lenye maendeleo mbalimbali.
Alisema
kuwa kutokana na jinsi gani Mbunge huyo anavyomsumbua juu ya suala la umeme
ameagiza kuwekwa kwa umeme katika vijiji vyote vya kata ya Miono bila kurukwa
kwa nyumba ya aina yeyote ile.
Aidha waziri huyo amemhakikishia Mbunge huyo
kuwa serikali kupitia wizara yake imekubaliana kupeleka umeme katika vijiji
vyote vilivyobaki katika jimbo hilo na jambo hilo lianze mara moja.
"Serikali ya awamu ya tano iko makini kuhakikisha wananchi wake wanapatiwa
huduma zote pasipo kuangalia itikadi ya kisiasa"
Aidha Dk Kalemani
amewataka wakandarasi kote nchi ni kuhakikisha wanawapatia ajira vijana
wanaozunguka miradi ili kurahisisha utendaji wa kazi pia kuwapatia fursa vijana
wa maeneo husika ambako miradi inapita.
Aliongeza
kuwa anatoa onyo kwa wakandarasi wanaochelewesha kuwaunganishia wananchi umeme
huku wakiwa wamesha maliza kulipia fedha zao za kuunganishiwa umeme ambazo ni
shilingi elfu 27 iwe Rea au Tanesco.